Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eliuterius Hyera, aliyekuwa Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi Chiungutwa wilayani Masasi, amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi na askari mwenzie.
Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicodemus Katembo leo Februari 03, 2024, imeeleza kuwa askari hao walikuwa kwenye jukumu la ukamataji wa mtuhumiwa anayedaiwa kuvunja ofisi (Haikutajwa) na kuiba.
“Mtuhumiwa huyo alianza kukimbia ili asikamatwe ndipo Askari aliyekuwa na bastola alipofyatua risasi kwa lengo la kufanikisha ukamataji na ikapelekea kumjeruhi Mkaguzi huyo.
Juhudi za kuokoa maisha yake zilifanyika kwa kupelekwa Hospitali ya Ndanda ambapo alifariki dunia akiendelea na matibabu.” Imeeleza taarifa ya ACP Katembo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi, huku mtuhumiwa akiendelea kushikiliwa kwa hatua zaidi za kisheria.
Source - CloudsTv
hivi haya magazeti bado yapo?Daah kichwa cha habari ni kama tukio la kukusudia habari za namna hii zinaandikwa magazeti ya Ijumaa...
Jeshi la polisi mkoani Mtwara Lina makando kando mengi,
Sijatafatilia sijui kama yapo ila nawajua miaka hiyo kichwa cha habari tofauti na habari yenyewe Mkuu..hivi haya magazeti bado yapo?
KabisaNadhani mods wangeweka kichwa cha habari sawa kuliko hivi kilivyo...
Yamewarudia wenyeweYale yale ya Aquilina
Umenikumbusha movie ya kamanda kwa marehemu Akwilina.Hatua za kisheria kwa maana alikosea kushika bastola au mhalifu alifanya dawa kugeuza uelekeo wa risasi
😆😆😆wanaishaje wakati wanauana wawili depo wapo 3000 bado mwezi waje mtaani!
ww endelea kukwapua simu za watu na piki piki watakushika tu siku moja.
Wakubwa waache Kutembea na Wake za Askari wadogo tafadhali kwani wenye Wake hubeba Roho za Visasi ambavyo huvisindikiza katika Matukio yatakayowabeba kuwa ni Oparesheni tu za Kijeshi ambapo Mmoja akifa / akiuwawa hiyo itaitwa ni bahati mbaya.Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eliuterius Hyera, aliyekuwa Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi Chiungutwa wilayani Masasi, amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi na askari mwenzie.