Asilimia 78 ya wafanyabiashara hawajui kodi wanatakiwa kulipa

Asilimia 78 ya wafanyabiashara hawajui kodi wanatakiwa kulipa

Luhamba II

Senior Member
Joined
Mar 22, 2025
Posts
126
Reaction score
186
Kwenye Thread hii nimekuandikia aina za Kodi unazotakiwa kulipa kama Mfanyabiashara nchini Tanzania.

1. Kodi ya mapato
Hapa Kuna Kodi aina mbili (Income Tax au Corporate Tax)
Hutegemea na aina ya biashara, hii hua ni 30% ya faida ya biashara au Kampuni.

2. VAT
Value Added Tax hii Kodi ambayo ni 18% ya thamani ya bidhaa au huduma. Hii ni Kodi ambayo hulipwa na biashara au Kampuni ambayo unauza zaidi ya Million 200 TZS.

3. Withholding Tax
Hii huitwa Kodi ya Zuio, ni Kodi ambayo hukatwa mapema kwenye mshahara au huduma.
Mara nyingi hua ni 10% lakini hutofautiana kulingana na Tax bracket.

4. Skills and Development levies
Hii hulenga kusaidia maendeleo ya ujuzi nchini.

5. Excise Duty
Hii ni Kodi ambayo hutozwa kwa bidhaa maalum kama Pombe, Sigara, mafuta na simu.

6. Property Tax
Hii hulipwa na makampuni yanayomiliki majengo. Hasa makampuni ya real estate.

Kodi zote hizi hutakiwa kulipwa kwa Wakati ili Kuepuka fine na Riba.

Hey, naitwa Luhamba Mimi ni mwanasheria na agency freelancer nawasaidia wafanya biashara kama wewe kusajili biashara leseni na Kampuni.

Kama unahitaji consultation zaidi kuhusu usajili wa Kampuni leseni na biashara unaweza kunitafuta WhatsApp au call kwa namba
0678131068.

Your Favorite Lawyer.
 
Back
Top Bottom