Afu hamkawihi kujiita GREAT THINKERS. Asha Migiro anahusiana nini na matamko ya Ban Kmoon. Maneno aliyosema Ban Kimoon ni kurudi Tangazo la Umoja wa mataifa kuhusiana na haki za binadamu,
The Universal Declaration of Human Rights.
Article ya pili ya tangazo hili inasema:
- Everyone is entitled to all the rights and freedoms set forth in this Declaration, without distinction of any kind, such as race, colour, SEX, language, religion, political or other opinion, national or social origin, property, birth or other status. Furthermore, no distinction shall be made on the basis of the political, jurisdictional or international status of the country or territory to which a person belongs, whether it be independent, trust, non-self-governing or under any other limitation of sovereignty.
The Universal Declaration of Human Rights
Azimio hii lilitungwa 1948 kabla Asha Migiro hajazaliwa. Mwaka 1984 serikali ya Tanzania ilifanya mabadiliko ya kikatiba na kutambua haki za binadamu. Soma kipengle hiki chini:
- (9) Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, amabyo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha-
- (a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;
- ---
- (f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu;
Hiyo hapo juu ni katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, SEHEMU YA PILI: MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI, Ibara ya 9, Kipengere (f).
Mambo aliyosema Ban Kimoon kulinda haki za mashoga yanakubalika na katiba ya Tanzania ya mwaka 1984. Na Tanzania ni signatory wa Tamko la Haki za Binadamu. Hivyo mnavyompinga Ban Kimoon na Mama Asha Migiro ni kutotumia akili kwa sababu serikali yenu ilikubali hayo.
Tumie akili na sio kutoa hoja kwa hisia.
Wenu
Za10[/QUOTE
KUMBUKA
Pamoja na Tanzania kuridhia UN Universal Declaration 1948, haikuridhia ushoga, na suala la kutambua haki za mashoga na wasagaji yamejitokeza juzi juzi katika moja ya mikataba ya kimataifa iliyopitishwa ambayo ilitaka wanachama kuridhia na Tanzania haijaridhia
Pili Katiba ya Tanzania pamoja na Sheria ya Ndoa, 1971 vinatambua ndoa ni kati ya mwanaume na mwanamke, sasa hicho unachokisema ndugu yangu umekitoa wapi
Tafadhali usitupotohse acha wanasheria waingie jamvini watujuze zaidi lakini mm nijuavyo convention ya kutambua haki za mashoga na wasagaji ss sio signatory