Aseme, asiseme, hayuko salama

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,727
Wana jamvi
Suala la Roma na utekaji wake na wenzake lina sura nyingi, lakini nawasihi tusisahau sura hii:
- Kwa kuwa aliweza kutekwa, hakuwa salama
- Kwa kuwa aliachiwa na watekaji bila kulazimishwa na nguvu yoyote - hayuko salama
- Akisema yote yaliyotokea tangu kutekwa kwake, hatakuwa salama
- Hata akikaa kimya kama alivyofanya, hayuko salama ( watekaji wanajuta kwa nini wamemwachia)

Formula nzima kuhusu utekaji huu ni kuwa: Majambazi wote na watekaji wote hukamatwa na serikali. Ukiona mtu kaiba, kaua au kateka, na asikamatwe, uje wazi kuwa mtekaji, muuaji, mwizi ni serikali yenyewe.
Hata serikali yenyewe hutamba kuwa ina mkono mrefu, leo hii inatuambia haijui. iNAHUSIKA.

Haya si mageni: Kamwulize Ulimboka, Kibamba, Kiongozi wa Vijana wa JKT waliodai ajira, Kiongozi wa wafanya biashara waliogomea mashine za EDF...
 
Back
Top Bottom