Asante....Vipi kuhusu umuhimu wake katika kukuza mahusiano?

PetCash

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
1,997
1,999
Habari za Asubuhi wadau wenye mapenzi mema na jamvi hili?

Leo nna jambo hili,
Neno Asante. Kwa kifupi mimi si mtu wa kutenda mema na kungoja shukrani kwa sababu naona hiyo si kutenda
wema tena bali ni biashara. Neno asante hapa kwenye kutendewa wema siyo shukrani bali ni neno tu linalotolewa
ili kumjulisha mtenda kwamba ume 'appreciate' alichotenda. Binafsi nisipoambiwa asante huwa najiuliza maswali mengi sana.
Labda hajaridhika na nlichotenda? kwa nini asiniambie haitoshi ili nimuongeze? Anataka nini hasa?
BTW : Kwa uchunguzi wangu, Watu wengi ambao wana tabia ya kutosema Asante ni Wenzi wetu(spouses) na ndugu (family).
Kwa hiyo mimi pasipokuwa na asante pananifanya nihisi labda nilichotenda hakitoshi...
Unajisikiaje ukiwa kwenye viatu vyangu?(put yourself in my shoes, as it appears to be!)
 
juzi kuna mdada nilimsaidia kitu, hata ahsante hakutoa. Iliniuma ila nikakumbuka tenda wema uende zako....


Pole bana dogo.........nayajua maumivu yake....... (ila ukweli mara nyingi wadada hawasemi asante..........sijui hatuoni umuhimu wake ama nini hata sijajua
 
"Asante" kwa upande wangu naona ina umuhimu sana. Huonyesha appreciation ya kitu ulichomfanyia mtu. Pia husaidia kudetermine kama mtu ameridhika na huduma au msaada ulioutoa au laaa.

Muda mwingine, ninapohisi nimemtendea mtu jambo jema nikakosa kupewa asante hujihisi kana kwamba msaada nilioutoa haukuwa na maana kwa mpokeaje au haukuwa na kiwango stahili au pengine mpokeaje hakuridhika na msaada niliotoa.

Kiungwana, nafikiri tujifunze kutoa asante kwa jambo lolote lile zuri ulilofanyiwa na mtu whether ni kwenye mahusiano ya wawili, marafiki, ndugu nk. au kwenye shughuli za kawaida za kila siku.

Asante.
 
Pole bana dogo.........nayajua maumivu yake....... (ila ukweli mara nyingi wadada hawasemi asante..........sijui hatuoni umuhimu wake ama nini hata sijajua

wadada wengi dharau na pozi. Unajua watu wenye dharau wengi wazito kushukuru. Ukimfanyia wema anaona unajipendekeza au ni wajibu wako au asiridhike na ulichofanya. Katika mazingira hayo kushukuru ni ngumu.
 
wadada wengi dharau na pozi. Unajua watu wenye dharau wengi wazito kushukuru. Ukimfanyia wema anaona unajipendekeza au ni wajibu wako au asiridhike na ulichofanya. Katika mazingira hayo kushukuru ni ngumu.


Daah! Ngumu kumesa......lakini ndio ukweli wenyewe...... wee nae mi nimekunong'oneza na we umeweka ngoma uwanjani......khaa!!
 
Daah! Ngumu kumesa......lakini ndio ukweli wenyewe...... wee nae mi nimekunong'oneza na we umeweka ngoma uwanjani......khaa!!

hahahaha! Mambo hadharani. Hakuna kumung'unya maneno hapa. Lol
 
Ni neno gumu sana kwa baadhi ya watu kulitoa
Kuna watu ambao huwa hawaoni umuhimu wa lolote ulilomfanyia hata kama umejitoa kwa namna gani
Kuna mengi utajiuliza iwapo uliyemtendea jambo hatatoa asante mfano ni kwamba hakuridhika na nililofanya au hakupendezwa na nililofanya au ni kwamba nimefanya vibaya kwa kiwango ambacho hakutegemea
Kwangu ni neno muhimu sana kulitoa au kumpa mtu hata kama alichokifanya hakifikii kiwango kile ambacho nilitegemea
Na ni neno zuri sana unapompa mtu Asante kwa kile ulichofanya hata kama ni kidogo
 
kuna bro. wangu mmoja akikupa kitu usiposema asante anakwambia kwani ulidhani ni wajibu wangu? then sahau kupata siku nyingine!!
 
Ahsanteni wanajamii kwa mchango wenu hapa sredini, Ahsante pia kwa wale waliosoma na kupita zao
 
Back
Top Bottom