Asante Mungu, hatimaye Mwenyekiti wa CCM, Dr. Magufuli, ameishiwa pumzi, hana pa kushika. Mimi nilijua mapema

Mkuu wetu wa nchi H.E J.P.Magufuli anaifanya kazi yake vizuri sana tena sana, Tatizo kubwa ni misinformation anazopewa na communities zake zinazomsaidia, Ukiangalia kwa jicho la tatu Mkuu ana nia ya kutupeleka Pazuri kabisa ila watu wanaomzunguka ndio chanzo cha mkwamo huu unaotokea.
Kwa maana hiyo tangu aingie madarakani yeye amekuwa wa kupotoshwa na hao wasaidizi wake tu? Kama ndo hivyo ina maana yeye hana uwezo wa kitambua kuwa anapotoshwa karibia kila afanyalo? Kama ndivyo basi tutakuwa na madhara makubwa sana ya kuongozwa na mtu anayeshikwa mkono na kuongizwa na wengine ( sikumbuki vizuri mtu huyo huwa anaitwaje)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wetu wa nchi H.E J.P.Magufuli anaifanya kazi yake vizuri sana tena sana, Tatizo kubwa ni misinformation anazopewa na communities zake zinazomsaidia, Ukiangalia kwa jicho la tatu Mkuu ana nia ya kutupeleka Pazuri kabisa ila watu wanaomzunguka ndio chanzo cha mkwamo huu unaotokea.
Samahani najua unakwazika lakini ameondoa watu makini kitengoni ameweka green guard unategemea nn na bado hata watu wachapakazi kaweka pembeni,ila mwisho upo karibu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naskia mahiga anapata tabu sn huko ughaibuni, mabeberu hawamuelewi kabisa na wao wameamua kutumia kile kikokotoo cha kukata walichokitumia ccm kumkata lowasa, misaada wamekata, Huduma ya mama kwa mtoto imekatwa kwakuwa wao ndio walikuwa wafadhili. Fao la uZazi wamekata, naskia katakata itaendelea zaidi siku zijazo, madurooooo njooo huku mwenzako yuko hukuuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naskia mahiga anapata tabu sn huko ughaibuni, mabeberu hawamuelewi kabisa na wao wameamua kutumia kile kikokotoo cha kukata walichokitumia ccm kumkata lowasa, misaada wamekata, Huduma ya mama kwa mtoto imekatwa kwakuwa wao ndio walikuwa wafadhili. Fao la uZazi wamekata, naskia katakata itaendelea zaidi siku zijazo, madurooooo njooo huku mwenzako yuko hukuuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Acc ya p4r imefungwa na bado

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bunge live,
Manunuzi
Sheria kandamizi za mitandao
Kuzuia local channel
Kuminya demokrasia
Tumbua tumbua
Kuwatumia mafarisayo wa dini
Sasa Sheria za kuuwa vyama vingi vyoote vimeshindwa pandisha asilimia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam,

Mzee Magufuli kaishiwa pumzi mapema sana.. nakumbuka matendo na mikwara yake ya 2016 na sasa ni tofauti kabisa. Kaishiwa pumzi, kalegea sana kisiasa. Anatamani Polisi, Jeshi, mgambo, magereza wote wamuunge mkono waziwazi kutokomeza Uwazi, uwajibikaji na na kuhakikisha nchi haina demokrasia.

Jikumbushe hotuba yake, kila mtu alijua kapata rais=>Hotuba ya Rais Magufuli akifungua rasmi bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Novemba 20, 2015 - JamiiForums

Anatamani kuona Mahakama inawaadhibu wapinzani wake wote wa kisiasa na wale wanaomkosoa wanafungwa Maisha, anatamani kuona kila mtu anampigia makofi kwa anachokofanya hata kama hakifai. Anatamani afananishwe na Nyerere. (Nyerere aliunganisha taifa, yeye wanasiasa wasio CCM ni adui wa nchi) hawawezi fanana katu.

Soma;

Rais Magufuli aingilia uhuru wa Mahakama, aagiza Jaji Mkuu amalize kesi za kodi Serikali ipate hela zake mapema - JamiiForums

Rais Magufuli awaagiza RPC na RC wa Njombe, kuwafungulia kesi upya watu walioachiliwa huru na mahakama, Jaji Mkuu na IGP wahakikishe amri inatekelezwa - JamiiForums


Baada kuona kashindwa kaanza kusingizia Mabeberu, kwani wakati wa Kikwete Mabeberu hawakuwepo?

Eti vyama vya upinzani visifanye kazi za kisiasa(Siasa hazifanyiki na anachofanya hakionekani), vifunge Ofisi ili nchi isonge mbele na iwe donor country. Hata baada ya miaka mitatu uongozi wake haujaweza kusaidia japo makazi bora kwa wazee wanaoishi mazingira Magumu na Vituo vya kulelea Wazee.

Rais Magufuli: Hakuna siasa mpaka 2020 - JamiiForums

Mwigulu: Marufuku ya mikutano ya siasa iko pale pale - JamiiForums

Tangu apate madaraka hadi leo, hotuba zake hazibadiliki, ni zilezile miaka yote mitatu hadi kila mtu anajua ataongea nini. Utasikia;

Tuna fedha za kujiendesha kwa miezi mitano bila kufanya kazi, Stiegler's Gorge, mapato kuongezeka kutoka bil 800 hadi tril 1.3 kwa mwezi, Watoto waliojiandikisha la kwanza wameongezeka, Wafanyakazi na vyeti hewa, Nchi yetu ni tajiri sana, Hapa kazi tu, nitawafanyizia kazi nk. Hakuna jipya,anarudia hayo hayo miaka yote mitatu ya Uongozi wake.

Hii ndo dalili ya kwamba mzee mkubwa kakwama na hajui kama kakwama.

Mei Mosi 2018: Rais Magufuli atapandisha Mishahara miradi mikubwa ya Serikali ikikamilika, Mwaka jana alinukuliwa Vibaya - JamiiForums

Huyu mwenyekiti wa CCM lakini utasikia.. Hii nchi yetu imeliwa sana, mtu unajiuliza kabla ya uongozi wake chama gani kilikuwa madarakani? Ni CCM? na yeye ni wa CCM?

Yaliyobaki ni kujisifia tu eti najua kuna mtu sehemu fulani kafanya kitu fulani. Sijui najua wanaoiba dhahabu sisemi sana kesi zipo mahakani. Sijui nina degree ya Korosho hadi sasa chuo kikuu hawajanipa certificate. Hahahaa...Wafanyabiashara wasiponunua korosho ntazinunua kwa siku tatu tu. Tunajenga SGR itakuwa Korosho. Kila mtu anajua.. Sijui nalala na mafile kitandani.

Rais Magufuli: Tutanunua Korosho kwa Tsh.3,300/=, JWTZ ihakikishe kila ghala linalindwa na Wakulima wanalipwa haraka bila usumbufu - JamiiForums

Alijifanya mzalendo eti dada yake asiende kutibiwa nje, Mungu akampenda zaidi. Sijajua mama yake kama kashasafirishwa.

Ukitaka abadilishe sura muulize haya maswali. Hata usiulize, just andika facebook haya maneno.

1. Trilioni 1.5 ipo wapi?, kwanini thamani ya shilingi imeshuka, kwanini hamna ajira wakati anadai pesa zipo

2. Ni sheria ipi anatumia kukataza vyama vya siasa kutofanya siasa.

3. Uchunguzi wa waliomshambulia Tundu Lissu, Alfonce Mawazo, Ben Saanane, Azory Gwanda.

4. Wanafunzi wengi wanaojiunga la kwanza wakimaliza la saba wataenda wapi?

5. Kwanini anaamulisha Polisi wakamati raia na kuwafungulia kesi na kuagiza Jaji mkuu na Polisi kuhakikisha wanafuatilia. Anatumia Sheria ipi?

6. Watu waliopotea kibiti, tume ya uchunguzi itaundwa lini?

7. Kwanini Tanzania hakuna Demokrasia?

9. Mgogoro wa Uchaguzi Zanzibar

10. Kwanini wanaomkosoa wanakamatwa?

My brother, jua utaishi bila furaha japo utajaribu kuuliza hayo maswal. Utaambiwa wewe sio Mzalendo, Utaambiwa wewe sio raia, utaambiwa wewe unatumikia mabeberu. Watatu watakutishia kukuua na hata ukitoa taarifa Polisi haitafanyiwa kazi.

Apandishwa Kortini kwa kumhusisha Rais Magufuli na sakata la trilioni 1.5/- - JamiiForums

Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali - JamiiForums

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali - JamiiForums

Jamaa alijua kuongoza Tanzania ni rahisi kama kusukuma mlevi.

Kwa haya anayofanya, mimi namuelewa, sababu bila hivyo atapaugua presha na kisukari. So bora nchi iendeshwe kidikteta ila anapokosea asiulizwe na atakayeulizwa atafutwe popote alipo.

Hii ni mbinu inatumika sana hata kwenye Ugomvi. Mtu akishindwa kupigana, anang'ata. Muacheni mwenyekiti wetu wa CCM ang'ate ili aonekane ameshinda.

Upo uwezekano mkubwa sana 2020 huyu mwenyekiti wa CCM anaweza asigombee Urais tena.

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea - JamiiForums

PhD ya Magufuli na wanasiasa wengine zichunguzwe upya! - JamiiForums
Ma DC na RC sheria inawaruhusu kuweka ndani masaaki 48, tumie sheria hii ili watu wakati.

Majuzi....Ma DC na RC mnatumia vibaya sheria ya kuwaweka watu ndani bila kuwapeleka mahakamani. Acheni taiba hii😁😁😗😗🙂🙂
 
Watendaji wengi ni waoga kwake, Ila mkulu ana mawazo mazuri sana

Sijaelewa kwanini Magufuli anapenda utawala wa vitisho, amefanya hivyo kwa Bunge pale alipowatisha kuwa angelivunja bunge pale walipotofautiana nae na juzi nimemuona akiwatisha majaji wa mahakama pale walipoapishwa!!! Hotuba yake iliashiria kuwakumbusha majaji kuwa yeye ndio mkuu wao kwa vile anapelekewa majina na yeye anayachuja na kufanya uteuzi wa mwisho hivyo ni vyema wakakumbuka hilo, ili maamuzi yao yalingane na ustashi wake na chama chake. Hilo aliliweka wazi kwa kuwaeleza kuwa anafuatilia hukumu wanazozitoa mahakamani!!

Naona mwenendo huu wa kuwapandisha vyeo mahakimu na majaji ambao wanatoa hukumu za kupendelea chama tawala ni uingiliaji wa mhimili wa mahakama katika uhuru wake wa kufanya kazi kwa kutii katiba. It is tantamount to judicial intimidation. Sio jambo la busara kwa RAIS kutolea mifano hadharani ya hukumu za majaji zikiwa ndio vigezo vya kupandishwa vyeo.!!!
.
 
Back
Top Bottom