Mungu kweli si Athuman,
Baada ya kusoma comments mbalimbali humu kuelekea mechi ngumu ya Simba dhidi ya AS Vita, nilivunjka moyo mno kiasi cha kula chakula cha jioni na baada ya taarifa ya habari nikazima simu na TV na kukimbilia kitandani.
Saa 4.45 usiku nikachungulia YouTube nikaona bado simba haijafungwa halafu mtangazaji anasema Simba wamejitahidi na kwamba mechi ya mwisho katika uwanja ule muda kama huo Simba walikuwa wamekalia 3-0. Nikaona dharau dhidi ya Simba inaendelezwa kiaina.
Nikazima simu japo usingizi hakuna. Nilichungulia tena dakika kumi kabla ya mchezo kumalizika nikaona Simba 1 wenyeji wao 0. Nikajikaza kuangalia dakika zilizobaki hadi mwisho.
Nikiwa alone room kwangu niliamka kuwasha TV kana kwamba mechi ndo inaanza, nikaishia kuangalia hapa na pale kwa furaha ya ushindi wa Simba.
Kuna mchambuzi anajita Jeff, alisema kwamba kwa beki ile iliyocheza siku ya mechi kati ya Simba na Dodoma, Simba hawatafika mbali. Ni maoni yake, lakini tosha tu kusema kwamba asante kwa walioitabiria Simba mabaya kwa kuwa Mungu amewajibu utabiri wenu na roho mbaya haijengi hata siku moja. Isitoshe dua la kuku halimpati mwewe.
Simba imeanza hivi, inshallah mwenye Mungu aendelee kuisimamia hata katika mechi ya marudiano.
This is Simba. Not utopolo.