Kila mtu ana mbuyu wake. Mi sipendi hata kumsikia sanasana unapozungumzia suala la mikopo kwa wanafunzi. Aliwaathiri sana wadogo zangu na familia yangu alipotangaza kuwa wavulana wote waliopata dv II hawatapata mkopo ila itakuwa kwa wasichana waliopata one na two na wavulana waliopata div. one pekee, matamko hayo aliyatolea akiwa ziarani nchini China.
Na kibaya zaidi wakàti anatoa hilo tamko wanafunzi walikuwa wameshadahiliwa na mkopo wameshaomba na wana miezi zaidi ya mmoja vyuoni. Na kibaya zaidi walikuwa wanachukuliwa wanafunzi wa div. one waliofaulu masomo ya art+ dini halafu anaachwa wa div. two aliyefaulu masomo ya kawaida tena ya Economics na Hesabu.
Alifanya maamuzi mabovu kuwahi kupindukia katika tasnia ya taaluma Tanzania. Huyo kikwete unaemsema wewe kwa upande wangu naona hata kichefuchefu nikiona sura yake popote pale.