Asante Jaji Lubuva kwa matokeo ya 2015

Unadhani angekuwa rais angehama?
Urais ungekuwa kinga ya mali zake. Huko ccm kamsujudia shetani hivyo anapewa fahari za dunia hii.
Who knows anaweza kuwasujudia wazungu wakombe migodi yote ya madini?

Morani kimeo huyu.
 
Who knows anaweza kuwasujudia wazungu wakombe migodi yote ya madini?

Morani kimeo huyu.

Mzungu akitaka madini yako, umsujudie, usimsujudie atayachukua. Angalia Acacia inasemekana hawajasajiliwa hapa nchini na rais aliyepo madarakani hawasujidii lakini bado wapo na wanachukua madini. Mzungu ni kama maji, usipomnywa utamuogea. Kama huamini nenda Library Hapo chuo kikuu kaangalie vitabu vya wazungu ni vingapi na vya waswahili ni vingapi, kisha uje utoe mrejesho.
 
DECLARATION OF INTEREST: Mimi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa, wala sina utaalamu mkubwa wa mbinu za kisiasa. Mimi ni mtanzania huru na mwenye maoni huru.

Licha ya kazi iliyofanywa na sekretarieti ya CCM katika kulikata jina la Lowasa kwenye kinyang'anyiro cha wagombea wa urais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, watanzania wengi waliingia mkenge wa kumshabikia fisadi Lowasa baada ya kuhamia UKAWA.

Baada ya tuhuma zake nyingi za ufisadi wa mabilioni ya shilingi, mpaka chama chake kumtupa, tuliona jinsi ndugu Lowasa alivyohangaika kwa uchu wa kutaka urais hata ikabidi kutimkia CHADEMA.

Kwa uzee ule na uchovu aliokuwa nao huku akitetema hovyo, hata mimi nilishawishika kuamini huenda angetutoka punde.

Sifahamu kama ni mbinu za kiintelijensia na usalama wa taifa, au ni figisu, hatimaye Jaji lubuva akamfutilia mbali ndugu Lowasa kupitia sanduku la kura huku wafuasi wake wakiachwa macho kodo wakihuzunika kama makinda ya njiwa.

Wakati tukiwa tunastaajabu kwa butwaa, Magufuli akachanja mbuga kwa kasi mpaka ikulu na kutwaa mamlaka. Lakini kwa uchungu, UKAWA wakabaki na fisadi lao huku wasijue walitupe wapi.

Leo hii Lowasa katimkia CCM, na anasema amerudi nyumbani! Tunajifunza nini? Je, mwanasiasa ni mtu wa kuaminika?

Mtu anayeweza kuwasaliti watu million sita waliokesha kumpigia kura, kumdekia barabara, kumsapoti na kumshangilia, mpaka wengine wakavunjwa miguu na polisi?? Huyu mtu anafaa kuongoza nchi? Ana ajenda gani? Ana aminika vipi?

Asante Lubuva kwa kumfyekelea mbali huyu masai uchwara mwaka 2015. Haukukosea . Viva Lubuva.
shikamoo pesa

babawawili
 
Mzungu akitaka madini yako, umsujudie, usimsujudie atayachukua. Angalia Acacia inasemekana hawajasajiliwa hapa nchini na rais aliyepo madarakani hawasujidii lakini bado wapo na wanachukua madini. Mzungu ni kama maji, usipomnywa utamuogea. Kama huamini nenda Library Hapo chuo kikuu kaangalie vitabu vya wazungu ni vingapi na vya waswahili ni vingapi, kisha uje utoe mrejesho.
Haya bwana.
 
Ni sawa na ile hadithi ya samson alipomuua simba, baadae nyuki wakatengeneza asali kwenye mzoga wa simba. Yes, huenda ni kweli Magufuli alishinda kupitia mfumo mbovu.

Hata hivyo, bado ninaamini tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Lakini kwa Lowasa yule, ni heri walimfyeka.
Kwa hatua zake za sasa ni kweli hakuwa mgombea mzuri.
Lakini kwa tume hii inayotawaliwa na kuongozwa, na mgombea mojawapo au chama kimojawapo HAPANA. Hatuhitaji uchaguzi wa kiini macho, wakati matokeo yanajulikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawai kuona masai mbabaishaji kama lowasa kiukweli kavuruga sana upinzani kwa matuhuma yake ya wizi baada ya kuona haitwi tena fisadi kataka anabadli gia hewani eti karudi nyumbani!! alaaniwe mbowe na kamati kuu yake uchwara kwa kutuletea mgombea hewa
 
Ameipaka chadema matope yasiyofutika! Kama ni kinyesi, basi kinanuka sebule yote.
 
Sijawai kuona masai mbabaishaji kama lowasa kiukweli kavuruga sana upinzani kwa matuhuma yake ya wizi baada ya kuona haitwi tena fisadi kataka anabadli gia hewani eti karudi nyumbani!! alaaniwe mbowe na kamati kuu yake uchwara kwa kutuletea mgombea hewa
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom