Regnatus Cletus
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,114
- 959
DECLARATION OF INTEREST: Mimi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa, wala sina utaalamu mkubwa wa mbinu za kisiasa. Mimi ni mtanzania huru na mwenye maoni huru.
Licha ya kazi iliyofanywa na sekretarieti ya CCM katika kulikata jina la Lowasa kwenye kinyang'anyiro cha wagombea wa urais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, watanzania wengi waliingia mkenge wa kumshabikia fisadi Lowasa baada ya kuhamia UKAWA.
Baada ya tuhuma zake nyingi za ufisadi wa mabilioni ya shilingi, mpaka chama chake kumtupa, tuliona jinsi ndugu Lowasa alivyohangaika kwa uchu wa kutaka urais hata ikabidi kutimkia CHADEMA.
Kwa uzee ule na uchovu aliokuwa nao huku akitetema hovyo, hata mimi nilishawishika kuamini huenda angetutoka punde.
Sifahamu kama ni mbinu za kiintelijensia na usalama wa taifa, au ni figisu, hatimaye Jaji lubuva akamfutilia mbali ndugu Lowasa kupitia sanduku la kura huku wafuasi wake wakiachwa macho kodo wakihuzunika kama makinda ya njiwa.
Wakati tukiwa tunastaajabu kwa butwaa, Magufuli akachanja mbuga kwa kasi mpaka ikulu na kutwaa mamlaka. Lakini kwa uchungu, UKAWA wakabaki na fisadi lao huku wasijue walitupe wapi.
Leo hii Lowasa katimkia CCM, na anasema amerudi nyumbani! Tunajifunza nini? Je, mwanasiasa ni mtu wa kuaminika?
Mtu anayeweza kuwasaliti watu million sita waliokesha kumpigia kura, kumdekia barabara, kumsapoti na kumshangilia, mpaka wengine wakavunjwa miguu na polisi?? Huyu mtu anafaa kuongoza nchi? Ana ajenda gani? Ana aminika vipi?
Asante Lubuva kwa kumfyekelea mbali huyu masai uchwara mwaka 2015. Haukukosea . Viva Lubuva.