Ndugu;
1. Asali mbichi ni ile asali ambayo imerinwa moja kwa moja kutoka mzingani na kuchujwa tayari kwa matumizi, ndo asali ya kawaida(fresh);
Asali iliyoiva(pikwa) hii ni asali ambayo baada ya kurinwa huwa wanaipika/au kuichemsha, sasa sijajua wanaipikaje, lakini wanasababu za kuipika ambazo sijazijua vizuri, yamkini kutakuwa na matumizi yanayohitaji ichemshwe aghalabu katika kuihifadhi!
2. Nyuki wakubwa ndo hawa nyuki wa kawaida,
Nyuki wadogo ni vidudu fulani vidogo vidogo mithili ya mbu, navyo vina asali fulani hutengeneza na mara nyingi hukaa mapangoni, asali yao ni angavu kama maji na ladha yake ni tofauti na nyuki wakubwa, hupatikana kwa uchache maana ni vidudu vidogo sana.