ARUSHA: Zaidi ya tani 70 za sukari zagawiwa kwa wananchi

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Jumla ya tani 78 za sukari ambazo zilisalimishwa na baadhi ya wafanya biashara wa kubwa wa sukari katika jiji la Arusha zimegaiwa kwa wananchi wa wilaya ya Arusha mjini ambao walikuwa wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa sukari .

Sukari hiyo ambayo ilisalimishwa na wafanyabiashara wakubwa ambao ni Neema Investment imegaiwa katika jumla ya kata 25 zilizopo katika wilaya ya Arusha mjini huku kila kata ikiwa inapatiwa mifuko 1000 kwa ajili ya wananchi wake .

Akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arusha ,Afisa tarafa wa kata ya Suye Felician Mtahengerwa alisema kuwa sukari sukari hiyo inayogaiwa kwa wananchi ni ile ambayo iliingizwa hapa mkoani na baadhi ya wafanya biashara wakubwa na kuisalimisha katika ofisi ya mkuuwa mkoa kama agizo lilivyotolewa .

Alisema kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha alisema kuwa mfanya biashara yeyote wa sukari ambaye anaingiza sukari mkoani hapa anapaswa kutoa taarifa katika ofisi yake kabla ya kufanya kitu chochote ikiwemo kabla ya kuuza sukari hiyo ivyo wafanyabishara hawa waliisalimisha sukari hiyo na ndio ambayo inagaiwa kwa kufuata utaratibu.

Alisema awali walishagawa sukari tani 45 na sasa ivi wanagawa tani zingine 33 ambazo zimetoka kwa mfanyabishara Neema intaprasesi ambayo yeye aliingiza sukari hii mara baada ya serekali kutoa agizo hivyo aliamua kuisalimisha kwa kutoa taarifa katika ofisi ya mkuu wa mkoa na sasa ivi ndio wameigawa .

“kunautaratibu wa wafanyabishara wakubwa wanapoingiza sukar I tu hapa mkoani kutoa taarifa sehemu husika ili sukari ile iweze kugaiwa kwa kufuata utaratibu hivyo huyu alitoa taarifa na ndio maana tumekuja hapa kuungana nae kuakikisha kila kata inapata sukari mifuko 1000 ambayo itauzwa kwa bei halili ya serekali ambayo imeelekezwa”alisema Mtahengerwa.

Alisema kuwa utaratibu huu unaotumika wa kugawa sukari utaendelea hivi hivi na hata sukari ambayo imeagizwa na waziri mkuu iwapo itafika utaratibu huu huu ndio utatumika adi pale tatizo la sukari litakapo malizika kabisa

Alitoa wito kwa wafanyabiashara wakubwa ambao wanaingiza sukari kutoa taarifa katika ofisi husika kwani wakiingiza bila kutoa taarifa iwapo wakibainika watachukuliwa hatua ya kisheria ikiwa ni pamoja na kutaifishiwa sukari yote.

Aidha pia aliwataka wafanya bishara wadogo wadogo ambao wamepata sukari hiyo kuuza kwakufuata bei elekezi kwani wanapokiuka agizo hilo iwapo watabainika wameuza kwa bei ya juu tofauti na bei elekezi sheria kali watachukuliwa ikiwemo ya kuwapeleka mahakamani.

Kwa upande wake mfanyabishara mkuu ambaye alijitambulisha kwa jina la Romanusi Mwacha alisema kuwa yeye kama mfanyabishara mkubwa ameamua kumuunga Rais Magufuli mkono kwa kuanza kuuza sukari kwa bei elekezi japo kuwa amepata hasara kubwa.

Alisema kuwa kama yeye amenunua sukari shilingi 1900 kilo na bado ajaweka bei ya usafiri kutoka aliponunua dar adi hapa lakini kutokana na agizo la serekali ameamua kulifuata na kumuunga magufuli mkono na ndio maana pamoja yakuwa amenunua bei gali lakini anauza bei raisi kwa kilo shilingi 1700 ili mfanyabiashara mdogo anaenunua aweze kwenda kumuuzia mlaji bei ya shilingi 1800 kama serekali ilivyoelekeza.
Aliwasihi wafanyabishara wengine ambao wameficha sukari wazitoe na wale ambao wanauza katika maduka ya reja reja wauze bei elikezi ili kutoweza kumuumiza mlaji ambaye ni mwananchi .
 
Haya intapraisesi, nilifikiri mnagawa bure.
Mbona hiyo sukari yenyewe haipo?
hivi hili neno Bure nadhani linatumika vibaya.

Semeni hukweli sukari inauzwa na siyo kugawiwa kwa wananchi.

Hapa naomba hili jambo liwekwe vizuri, maana linaleta mkanganyiko kwa wananchi.

Unakuta mwananchi Anakwenda akidhani anagawiwa bure. Alafu anaambiwa lete fedha!
 
Sio maigizo tu ni pamoja na ujinga,yaani wanataka kuturudisha enzi za Ujamaa na Kujitegemea ili ULANGUZI NA MWENDO WA KURUKA virejee tena au?,jibu pekee kwa matatizo ya UHABA ni kuondoa UKIRITIMBA na UMANGIMEZA,yaani watu wapewe uhuru wa kuagiza bidhaa zote muhimu kutoka nje bila kuleta UHARO wa KULINDA VIWANDA NCHINI ambavyo viko TAABANI na vimejaa MAJITU MAVIVU YASIO NA TIJA kwa serikali wala wananchi,ACHA WENYE PESA ZAO WAINGIZE BIDHAA ZOTE NA USHINDANI WA KIBIASHARA UTATOKEA NA WANANCHI WATAFAIDIKA.
 
Ukweli
 
Uko sahihi, kwa upande wangu NASEMA KWA SAUTI KUWA Magufuli anahatari ya kuvurunda zaidi ya maraisi wote tz.
Hadi sasa wafanyabiasha, watumishi wa umma na wawekezaji hawana imani naye kwani hawajui KESHO ataamka na kauli gani yenye madhara na hatima zao.
Ninamuunga mkono kwa nia ya kupinga ufisadi lakini vjaridhishwa na utekelezaji wake naona utaleta madhara makubwa nchi hii.
Pia sijaelewa vizuri shabaha au malenga kuifikisha wap tz na watanzania kiuchumi na kwa mbinu gani. Ninashuhudia matamko na ushtukizaji wa kila mara na bado sio matokeo chanya zaidi ya kuleta mkwamo wa kiuchumi.
Kitendo cha kudhamiria kushusha badala ya kuongeza mishara nalo ni tatizo kubwa kwani linashusha ari ya kazi.
 
Yaani tunashangilia ooh eti MAJIPU yanatumbuliwa,kumbe tunakaribisha SARATANI ya UBONGO.Sijawahi kuona nchi ambayo inazuka ghafla ooh eti KIBALI CHA KUAGIZA SUKARI kutoka nje kinatolewa IKULU,wehu mtupu,,..yaani ni kutngeneza ULAJI na RUSHWA iliokithiri,.ETI ANATUMBUA MAJIPU.
 
Jumla ya tani 78 za sukari ambazo zilisalimishwa na baadhi ya wafanya biashara wa kubwa wa sukari katika jiji la Arusha zimegaiwa kwa wananchi wa wilaya ya Arusha mjini ambao walikuwa wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa sukari .

Sukari hiyo ambayo ilisalimishwa na wafanyabiashara wakubwa ambao ni Neema Investment imegaiwa katika jumla ya kata 25 zilizopo katika wilaya ya Arusha mjini huku kila kata ikiwa inapatiwa mifuko 1000 kwa ajili ya wananchi wake .

Akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arusha ,Afisa tarafa wa kata ya Suye Felician Mtahengerwa alisema kuwa sukari sukari hiyo inayogaiwa kwa wananchi ni ile ambayo iliingizwa hapa mkoani na baadhi ya wafanya biashara wakubwa na kuisalimisha katika ofisi ya mkuuwa mkoa kama agizo lilivyotolewa .

Alisema kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha alisema kuwa mfanya biashara yeyote wa sukari ambaye anaingiza sukari mkoani hapa anapaswa kutoa taarifa katika ofisi yake kabla ya kufanya kitu chochote ikiwemo kabla ya kuuza sukari hiyo ivyo wafanyabishara hawa waliisalimisha sukari hiyo na ndio ambayo inagaiwa kwa kufuata utaratibu.

Alisema awali walishagawa sukari tani 45 na sasa ivi wanagawa tani zingine 33 ambazo zimetoka kwa mfanyabishara Neema intaprasesi ambayo yeye aliingiza sukari hii mara baada ya serekali kutoa agizo hivyo aliamua kuisalimisha kwa kutoa taarifa katika ofisi ya mkuu wa mkoa na sasa ivi ndio wameigawa .

“kunautaratibu wa wafanyabishara wakubwa wanapoingiza sukar I tu hapa mkoani kutoa taarifa sehemu husika ili sukari ile iweze kugaiwa kwa kufuata utaratibu hivyo huyu alitoa taarifa na ndio maana tumekuja hapa kuungana nae kuakikisha kila kata inapata sukari mifuko 1000 ambayo itauzwa kwa bei halili ya serekali ambayo imeelekezwa”alisema Mtahengerwa.

Alisema kuwa utaratibu huu unaotumika wa kugawa sukari utaendelea hivi hivi na hata sukari ambayo imeagizwa na waziri mkuu iwapo itafika utaratibu huu huu ndio utatumika adi pale tatizo la sukari litakapo malizika kabisa

Alitoa wito kwa wafanyabiashara wakubwa ambao wanaingiza sukari kutoa taarifa katika ofisi husika kwani wakiingiza bila kutoa taarifa iwapo wakibainika watachukuliwa hatua ya kisheria ikiwa ni pamoja na kutaifishiwa sukari yote.

Aidha pia aliwataka wafanya bishara wadogo wadogo ambao wamepata sukari hiyo kuuza kwakufuata bei elekezi kwani wanapokiuka agizo hilo iwapo watabainika wameuza kwa bei ya juu tofauti na bei elekezi sheria kali watachukuliwa ikiwemo ya kuwapeleka mahakamani.

Kwa upande wake mfanyabishara mkuu ambaye alijitambulisha kwa jina la Romanusi Mwacha alisema kuwa yeye kama mfanyabishara mkubwa ameamua kumuunga Rais Magufuli mkono kwa kuanza kuuza sukari kwa bei elekezi japo kuwa amepata hasara kubwa.

Alisema kuwa kama yeye amenunua sukari shilingi 1900 kilo na bado ajaweka bei ya usafiri kutoka aliponunua dar adi hapa lakini kutokana na agizo la serekali ameamua kulifuata na kumuunga magufuli mkono na ndio maana pamoja yakuwa amenunua bei gali lakini anauza bei raisi kwa kilo shilingi 1700 ili mfanyabiashara mdogo anaenunua aweze kwenda kumuuzia mlaji bei ya shilingi 1800 kama serekali ilivyoelekeza.
Aliwasihi wafanyabishara wengine ambao wameficha sukari wazitoe na wale ambao wanauza katika maduka ya reja reja wauze bei elikezi ili kutoweza kumuumiza mlaji ambaye ni mwananchi .
Asante kwa taarifa
 
Uko sahihi, kwa upande wangu NASEMA KWA SAUTI KUWA Magufuli anahatari ya kuvurunda zaidi ya maraisi wote tz.
Hadi sasa wafanyabiasha, watumishi wa umma na wawekezaji hawana imani naye kwani hawajui KESHO ataamka na kauli gani yenye madhara na hatima zao.
Ninamuunga mkono kwa nia ya kupinga ufisadi lakini vjaridhishwa na utekelezaji wake naona utaleta madhara makubwa nchi hii.
Pia sijaelewa vizuri shabaha au malenga kuifikisha wap tz na watanzania kiuchumi na kwa mbinu gani. Ninashuhudia matamko na ushtukizaji wa kila mara na bado sio matokeo chanya zaidi ya kuleta mkwamo wa kiuchumi.
Kitendo cha kudhamiria kushusha badala ya kuongeza mishara nalo ni tatizo kubwa kwani linashusha ari ya kazi.

Mkuu jambilo ni wap huyu jamaa kapambana na ufisad? Tuwe wakweli serikali hii inapambana na watumish wa ngaz za chini au waliokuwa hawapo ktk chain yao mafisad wakuu mbona wanalala usingiz na kula vizur tu mi sina imani nae huyu hata kidogo maigizo mengi. Richmond na escrow hapa ndo pakuanzia mana hata serikali ya viwanda itahitaji umeme ukizungumzia tatizo la umeme na hasara kubwa ktk taifa hili lazima ukamue hapa!!!
 
hivi hili neno Bure nadhani linatumika vibaya.

Semeni hukweli sukari inauzwa na siyo kugawiwa kwa wananchi.

Hapa naomba hili jambo liwekwe vizuri, maana linaleta mkanganyiko kwa wananchi.

Unakuta mwananchi Anakwenda akidhani anagawiwa bure. Alafu anaambiwa lete fedha!
Sukari yenyewe iko wapi? Usanii mtupu
 
Back
Top Bottom