Arusha yaongoza viashiria vya rushwa

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Wadau kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi iliyotolewa na Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi Serikalini(PPRA) Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kuwa na Taasisi nyingi zenye viashria vya rushwa kwenye manunuzi. Ripoti hiyo imeshakabidhiwa kwa Waziri wa Fedha huko Dodoma na Dr Marten Lumbanga ambae ni mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo. Mheshimiwa Waziri wa Fedha ameagiza wahusika wote kutoka taasisi hizo wachukuliwe hatua kwa kupelekwa TAKUKURU.
Taasisi hizo zilizotajwa ni kama ifuatavyo:-
a)The Nelson Mandela Institute of Science and Technology.
b) Mamlaka ya Majisafi Arusha
c) Chuo cha Ufundi Arusha.
d) Chuo ya Uhasibu Arusha.
e) Arusha International Conference Center. (AICC)
Aidha taarifa hiyo ya ukaguzi itapelekwa baadae ili kujadiliwa bungeni.Ukaguzi huo ulifanywa katika Taasisi 17 nchini.
Karibuni
 
Arusha si inaongozwa na chadema nan kakwambia makamanda wanapenda rushwa?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…