ARUSHA: Wamiliki 9 wa nyumba wakiwemo viongozi wa dini wakamatwa kwa tuhuma za kuiba umeme

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Maafisa wa Shirika la ugavi wa umeme TANESCO mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamekamata zaidi ya wamiliki tisa wa nyumba wanaoiba umeme, vipuri vya kusambaza umeme na kuuza kama vyuma chakavu huku miongoni mwao wakiwemo watendaji wa serikali za vijiji na viongozi wa madhhebu ya dini.

Katika Operesheni hiyo maafisa wa TANESCO waliambatana na askari wa Jeshi la Polisi waliyofanikisha kukamatwa kwa baadhi ya watu na kuwafikisha kwenye kituo cha poilisi Usa Riva ambapo baadhi ya watuhumiwa walifanikiwa kutoroka na kutokomea kusiko julikana.

Mdhibiti wa mapato wa TANESCO mkoa wa Arusha Mhandisi Hasani Juma amesema maafisa wa TANESCO wameshangazwa na hatua ya baadhi ya watendaji wa serikali na viongozi wa dini ambao wana wajibu wa kusimamia na kukemea wizi nawo wamekuwa miongoni mwa wahujumu.

Mkuu wa kitengo cha mahusiano kwa wateja tanesco mkoa wa arusha saidi mremi amesema hakuna sababu ya watu wa maeneo ya vijiji kuunganisha umeme kienjyeji wakati gharama zake ni nafuu kuliko mijini na afisa usala akiomba jeshi la polisi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa watuhumiwa wanaoshikwa wakiiba viupuri vya usambazia umeme.

Chanzo: ITV
 
Sasa Hao ITV Wameshindwa Kuwaanika Majina Yahao Viongozi Wa dini Na Serikal Tuwajue
 
Wahakikishe hao 9 walio washikilia wanakuwa kwenye mikono salama.
 
Dunian kuna vituko jamen unaweza ukakuta m2 kwake anatumia umeme lakini hajaunganishiwa hiyo nmeishuhudia Arusha
 
Sasa Hao ITV Wameshindwa Kuwaanika Majina Yahao Viongozi Wa dini Na Serikal Tuwajue
Tatizo la Arumeru ni moja tu ...kwamba kila mkazi wa huko ana title ya Mchungaji hii ikisemwa kuwa ni laana ya kuwaua wamisionari na kufukua maiti zao kisa hazijatahiriwa.
 
Back
Top Bottom