Arusha Technical College(ATC) mnatatizo gani na wanafunzi wenu?

mkata majani

Member
Sep 12, 2019
9
7
kuna msanii mmoja wa bongo flava aliwahi kusema kuwa "vyote kushoto na kucheka kinyume chake ni kulia"
wanafunzi wa Arusha Technical College(ATC) waliamini mwalimu kutaka rushwa ya ngono kwa mwanafunzi ni kitendo kilicho kushoto na ivo wakataka kukiweka kulia(sawa),,,

wiki kadhaa zilizopita tulisikia tuhuma za rushwa ya ngono zilizokuwa zikikikabali chuo cha ATC,,, yule mwanafunzi alikuwa shujaa baada ya kulivumbua lile swala na kulitatua kwa namna ya kipekee,,, yule binti alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu diploma,,, wanafunzi wa ATC waliomaliza mwaka wa tatu diploma wamekuwa wakisubiri matokeo yao yapelekwe NACTE kwa takribani mwezi mmoja sasa bila ya mafanikio,,, wakihoji wanaambiwa field ndo imechelewesha matokeo kutumwa ilihali field iliisha toka tarehe 02/08/2019,,, ijumaa ya tarehe 13/09/2019 dirisha la mwisho la udahili TCU linafungwa na ivo kuwafanya hawa wanafunzi wenye nia ya dhati ya kutaka kusoma mwaka huu kusubiri mpaka mwakani,,, hata ikitokea TCU wakafungua dirisha lingine uwezekano wa chuo kutuma matokeo bado ni mdogo,,,

baada ya kuisikia hii stori kutoka kwa uyu muhitimu wa diploma kutoka ATC ndio nikamkumbuka yule msanii wa bongo movie aliyesema "kuna kupuliza ili iwake na kupuliza ili ipoe"

mwisho aliniuliza kama wataweza kulishinda ili swala kama walivyolishinda lile swala la rushwa ya ngono" kwasababu nilikuwa sina jibu la swali lake basi na mimi nikamuuliza kama anauhakika kuwa ile vita dhidi ya ngono waliishinda? na kama waliishinda je mpinzani/wapinzani wao walikubali kushindwa?
 
Back
Top Bottom