Arusha: Tani 33 za sukari zasalimishwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
sukari..jpg


Wakati watu tisa wameshakamatwa hadi sasa katika msako wa wanaoficha sura, mfanyabiashara mmoja kigogo mjini hapa amesalimisha tani 33 kwa mkuu wa mkoa.

Arusha. Wakati watu tisa wameshakamatwa hadi sasa katika msako wa wanaoficha sukari, mfanyabiashara mmoja kigogo mjini hapa amesalimisha tani 33 kwa mkuu wa mkoa.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa limekuwa likifanya msako huo ambao umebaini kuwa wafanyabiashara wote wanaouza sukari tofauti na bei elekezi.

Mfanyabiashara huyo, Romanus Macha asalimisha tani 33 za sukari zilizokuwa kwenye mifuko ya kilogramu 50.

Macha aliiambia kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya iliyokuwa kwenye msako huo kuwa ameamua kusalimisha sukari hiyo ili kutii agizo la Serikali kuhusu kupanga bei elekezi ya Sukari .

Alisema sukari hiyo ilifikia jana asubuhi na alishaitolea taarifa kwa mkuu wa mkoa na wa wilaya kuwa ana sukari

"Utaratibu ulioko sasa ni kwamba kama kuna sukari unatakiwa utoe taarifa kwa mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya, ili akupangie jinsi ya kuuza. Nilimsikiliza Rais wakati akiagiza hivyo na ndivyo nilivyofanya kabla ya sukari kuwasili," alisema Romanus.

Chanzo: Mwananchi
 
Wr

Wawekezaji walanguzi wa "kuagiza na kulangua" sukari hatuwahitaji hata kidogo.
sio kila muwekezaji na mfanyaqbiashara ni mlanguzi/muhuni
wengine wasafi,.
ila hii system mbovu itawakimbiza aiseeeeeeeee
hope ulimsikia sa100
 
sio kila muwekezaji na mfanyaqbiashara ni mlanguzi/muhuni
wengine wasafi,.
ila hii system mbovu itawakimbiza aiseeeeeeeee
hope ulimsikia sa100[/QUOTE
Walanguzi bora wakimbie tu, hawana faida na sisi kabisa.
 
Mimi naona hata hao wanaofuga ngomb'e ni wahujumu uchumi vipi leo nyama kilo ni elfu nane wakati wengi wao wana ngomb'e mpaka 1000 halafu hawataki kuchinja ni kama wanavicha nyama ili bei izidi kupaa ni majipu tu
 
Back
Top Bottom