Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Kisiasa: Arusha ni ngome imara ya CHADEMA. Lakini CCM bado iko imara na inaendelea kuendesha siasa zake za ndani na nje. Wananchi wa Arusha wanashiriki katika siasa za jiji hilo kama sehemu ya maisha yao za kila siku. Kimsingi,hakuna asiyefuatilia siasa pale na nchi nzima. Wana-Arusha ni wanasiasa wa kuzaliwa.
Kiuchumi: Arusha kuna uwekezaji wa kutosha kuanzia mdogo hadi ule mkubwa kabisa. Uchumi wa Arusha unaonekana kwa macho.Hata vijana wa kawaida kabisa ni watafutaji wasiochoka na wanajitahidi kujiepusha na uvivu usio na maana.Lakini kuna changamoto za barabara hasa za mitaa. Hizi bado hazijaimarishwa vya kutosha.
Kijamii: Wana-Arusha ni marafiki, wasemaji wazuri, na wakarimu. Arusha ni tulivu na salama. Kuna changamoto tu kama za Dar na kwingineko za madadapoa.
Kielimu: Sekta hii sijaisoma vizuri kwa muda niliokuwa pale.
Kimichezo: Wana-Arusha ni wafutiliaji na washiriki wazuri wa michezo.
Hongereni wana-Arusha na mtafute suluhisho la changamoto mlizonazo. Asanteni sana kwa kutu-host kwa uzuri Mawakili Wasomi wa nchi hii na nyingine.