Arusha na tatizo la umeme

Nyangomboli

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
3,501
1,955
Nduguzanguni, nilikuwa na kiziara uchwala huko HANDENI, SIMANJIRO, SAME , MWANGA pia KARATU. Kwa kweli nimeshangaa sana kuona huko mgao haupo na kama kuna tatizo la umeme basi ni la kawaida tu na si kama hapa kwetu ARUSHA. Swali langu ni kwa wenzangu wenye uelewa mpana kidogo juu ya mambo haya ni kwamba, umeme tunaotumia hapa ARUSHA ni chanzo tofauti na sehemu nilizozitaja? Hapa kwangu naona tangu kumi na mbili upo ila ni mdogo sana na hata sioni vizuri. Tatizo laweza kuwa nini jamani? MSAADA NAHITAJI NDUGU YENU ILI NIELEWE.
 
Wanalipizwa wananchi kwa kuchagua cdm, hiyo ndiyo ccm ya jk.
 
maeneo yote uliyoyataja matumizi yake ya umeme ni madogo sana so..hakuna haja ya kuweka mgawo kwao.. lakini sio Mwanza za Arusha....
 
Hamia maeneo ya Mianzini juu around njia ya kwenda Ilboru tumeunganishwa na line ya mochuari. Umeme haukatiki zaidi ya nusu saa! Au tafuta maeneo yaliyounganishwa na line ya ikulu ndogo karibu na mahakama kuu!
 
line ya Ikulu si ni uzunguni nitatakiwa kulipa usd 2000 kwa mwezi mkuu? Duh!
 
Nduguzanguni, nilikuwa na kiziara uchwala huko HANDENI, SIMANJIRO, SAME , MWANGA pia KARATU. Kwa kweli nimeshangaa sana kuona huko mgao haupo na kama kuna tatizo la umeme basi ni la kawaida tu na si kama hapa kwetu ARUSHA. Swali langu ni kwa wenzangu wenye uelewa mpana kidogo juu ya mambo haya ni kwamba, umeme tunaotumia hapa ARUSHA ni chanzo tofauti na sehemu nilizozitaja? Hapa kwangu naona tangu kumi na mbili upo ila ni mdogo sana na hata sioni vizuri. Tatizo laweza kuwa nini jamani? MSAADA NAHITAJI NDUGU YENU ILI NIELEWE.

Nilikuwepo hapo Arusha kikazi last wiki...hali hiyo hata mie imenishangaza kabisa,umeme unakatika muda wowote na kuwaka muda wowote wakijisikia TANESCO......Nimeshangaa kwa namna ambavyo wakazi wa Arusha wanavyozoea hali hii,nadhani kuna kitu wanapaswa kufanya kubadilisha hali hii,vinginevyo hali ni mbaya Arusha.
 
Back
Top Bottom