Arusha: Mwanafunzi mbaroni kwa kuwatukana Rais wa Zanzibar, Mkuu wa Majeshi

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Mwanafunzi Mbaroni Kwa Kumtukana Rais Wa Zanzibar Dkt.shein Pamoja Na Mkuu Wa Majeshi Mwamunyage.

Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.

Akiongelea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu majira ya saa 09:00 asubuhi.

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe nje ya nchi huku hakuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.

“Mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya 'Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti' hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “ alisema Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtumiwa huyo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo, ”Dr. Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook."

Mkumbo alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka sheria na taratiu za kisheria.

Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yake.

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Isaac Emily (40), mkazi wa Olasiti jiji hapa inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakiku mkazi Arusha.

Swali langu;
Je, hayo ya Mwanafunzi huyu ni sahihi au ndio matumizi sahihi kuhamasisha machafuko kwa kivuli cha uhuru wa kutoa habari?
 
Yaan tumetoka kwenye uchaguzi juzi tu hapa hata hatujapumzika na JPM ndo anatekeleza Ahadi zake tena kanatokea kashenzi Fulani kanachochea MKUU WA MAJESHI apindue nchi? hivi anajua maana ya nchi kupinduliwa au anaandika tu? kwanza nani aliwambia Mkuu wa Majeshi kazi yake ni kupindua nchi? kwa cheo chake Mkuu wa Majeshi hawezi kupindua nchi, kuna situation ambazo zinaweza kumfanya CDF achukue nchi kama ile ya Misri, lakini kwa mazingira ya Tanzania hizo situation za Misri hazipo kabisa.
 
facebook
jamiiforums
twita
instagram
whatsap au chuoni kwao?

alitumia njia gani kati ya hizo
 
Kwahiyo mkuu wa majeshi naye kweli angeshawishika kupindua nchi kwa ushauri wa Harold?

Mtu unapokuwa busy na shughuli zako huna hili wala lile, afu mtu akaja kukupa taarifa Fulani au akakushtua tu, utapata "Hisia au hali gani"?

Ni kama mtu ulikuwa huna hili wala lile, mara "paaaa! unapewa wazo Fulani, utafanyaje? nataka nikufikirishe kidogo na wewe uweze kuona athari zake.
 
Unamshikilia mpaka ushahidi utakapokamilika?Aisee una si zaidi ya saa 24 uwe umemfikisha mahakamani,otherwise muachie huru na endelea na uchunguzi wako!kwann ukamkate mtu bila kukamilisha uchunguzi?Tena mtu ambaye unaona kwa mazingira hawezi toroka?Au na wewe hazikutoshi?
 
Zanzibar ni nchi kamili yenye raisi wake kama ilivyo marekani nk Hicho kitoto mambo ya nchi nyingine yanakihusu nini? Matatizo mengine ya kujitakia.Hicho kitoto kule Zanzibar hakiruhusiwi hata kupiga kura!!! Wala hakina kitambulisho cha Mzanzibari

Kinaendeshea uchochezi wake Tanzania bara !!! Wazanzibari wenyewe wako kimya chenyewe mdomo juu.Pilipili ya shamba inakiwashia nini? Wazanzibari wenyewe hawajatamka hayo kiliyotamka.hako katoto vipi?
 
Mwanafunzi Mbaroni Kwa Kumtukana Rais Wa Zanzibar Dkt.shein Pamoja Na Mkuu Wa Majeshi Mwamunyage.

Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.

Akiongelea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu majira ya saa 09:00 asubuhi .

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe nje ya nchi huku akuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.

“Mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya ,Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti,hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtumiwa huyo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo,”Dr Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama facebook."

Mkumbo alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka sheria na taratiu za kisheria .

Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yake.

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Isaac Emily (40), mkazi wa Olasiti jiji hapa inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakiku mkazi Arusha.

Swali langu;
Je, hayo ya Mwanafunzi huyu ni sahihi au ndio matumizi sahihi kuhamasisha machafuko kwa kivuli cha uhuru wa kutoa habari?
Ni kweli haya maneno ni mazito sana ila ninadhani huu ni utoto na unawezekana kuwa unachangiwa na sisi kuandika mambo pasi na kupima kwanza tukijidanganya kuwa ni haki yetu ya msingi kuongea/andika bila ya kubanwa.
Hakuna nchi yoyote ile duniani ambayo kuna haki hiyo.
 
Back
Top Bottom