Arusha: Mpaka wa Kenya na Tanzania, Namanga wafungwa

Hili huenda lina ukweli. Week kadhaa zilizopita nilipita hapo Namanga kutokea Nairobi aisee upande wa Tanzania kuna Roadblocks sio chini ya nne hiyo yote ni kusaka wakenya tu. Nilishangaa kule Kenya hakuna kitu km hicho.
Labda siku hizi tu, Wakenya those days walikuwa wanakamata sana Watz hasa wakigundua huna hati wanazuia mpaka gari lisiondoke inabidi mwenye gari akufuate unarudi upande wa kenya unapigwa lock up kiana alafu kila mmoja anatolewa kwa buku 3
 
diplomasia diplomasia ! raisi yupo busy kukamata mchanga wa dhahabu bandarini msimsumbue, waziri mkuu anashughulika na kifaru aliyefariki selous na kesho raisi anaenda kuwafumania wanaolala gesti mchana wakati wa kazi
 
Sawa sheria za uhamiaji zifuatwe kama kawaida na kama hao Wakenya waliokamatwa wakatiwa ndani hawakufuata sheria inayowapa uhuru wa kuishi Tanzania walisitahili adhabu kali zaidi ya hiyo bila kujali kuwa mimi naishi mpakani au la!, Na cha ajabu hao Wakenya waliokuwa wanaandamana walikuwa na sababu za kuandamana au walifuata mkumbo tu bila kujua kama waliokamatwa walivunja sheria.
 
Sawa sheria za uhamiaji zifuatwe kama kawaida na kama hao Wakenya waliokamatwa wakatiwa ndani hawakufuata sheria inayowapa uhuru wa kuishi Tanzania walisitahili adhabu kali zaidi ya hiyo bila kujali kuwa mimi naishi mpakani au la!, Na cha ajabu hao Wakenya waliokuwa wanaandamana walikuwa na sababu za kuandamana au walifuata mkumbo tu bila kujua kama waliokamatwa walivunja sheria.
Tanzania ilisaini mkataba wa free movement of persons Afrika Mashariki. Utekelezaji umetushinda.
 
Nyie mnaripoti habari mbaya tu msifiki mna uhuru huo.
wewe si uripoti habari nzuri tuchangie.

huna tofauti na boss wako anayetaka wandishi wa habari wamwandike yeye kwenye front page halafu wamsifie hata kama anachokifanya ni uchuro. kakasa mvuto kama bar-maid.
 
wanapoteza muda kufuatilia kwenye mitandao kumeandikwa nini, au waje na sinema ipi ya kuteka wananchi
Rais anashinda kwenye mitandao ila hataki wengine watumie mitandao ya kijamii roho mbaya haijawaki kutokea.
wengine wafanye kazi yeye kutumbua na kuteua hiyo nayo kazi?
 
Mipakani lazima jambo hili linaweza tokea wale kuingia huku kidogo na wa huku kuingia huku kidogo duniani kote ipo hivyo na nchi husika huwa hazina mashaka kwa vile uraia wao unajulikana ata kama wanaishi upande wa mwengine
 
Mipakani lazima jambo hili linaweza tokea wale kuingia huku kidogo na wa huku kuingia huku kidogo duniani kote ipo hivyo na nchi husika huwa hazina mashaka kwa vile uraia wao unajulikana ata kama wanaishi upande wa mwengine
vilevile watu wengi wa mipakani wengi ni kabila moja, ndugu moja au wameoona, wanamiliki mashamba(mali) upande wa pili na marafiki wa muda mrefu, kwa hiyo inahitajika umakini wa hali ya juu ku-deal nao la sivyo utajenga uhasama au lolote laweza tokea.

anyway mbona wachina, waarabu, wahindi, wasomali, wanaigeria wamejaa kariakoo kwa nini wasianze na hao unaenda kupambana na ndugu wamoja?
 
Tatizo Rais ndo waziri wa mambo ya nje mpaka atoe tamko mawaziri wapo tu kama geresha
wee! humwonei waziri huruma unataka atumbuliwe asubuhi na mapema, kumbuka hata miaka miwili hajatimiza, matamko yote anayatoa Rais sio vinginevyo mbaya zaidi la kimataifa.
 
uchunguzi ufanyike kujua chanzo ni nini wahusika walioko kwenye mpango huu ni akina nani nani alibeba petrol, nani aliwasha nani aliharibu transformer nani kamtuma aharibu rasilimali za nchi na kuleta taharuki hatua kali zichukuliwe dhidi ya uhalifu huu wa Amani wa jumuia ya afrika mashariki .
 
Tanzania ilisaini mkataba wa free movement of persons Afrika Mashariki. Utekelezaji umetushinda.
Ni kweli mpango huo nadhani bado utekelezaji wake haujaanza na wakati huo wanajaribu kuangalia athari zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji huo.
 
Wakuu, Ni kweli kuwa kwa sasa pale mpakani Namanga umefungwa, wakenya wamegoma na wamefunga mpaka sababu ni serikali ya Tanzania pale mpakani kuwanyanyasa wakenya wanaoishi mpakani pande za Tanzania.

Wikiendi hii waliwashika wakenya 12 na kuwafungia.

Watu wanaandamana na tangu asubuhi hakuna gari wala mtu anayevuka mpaka.

View attachment 487450 View attachment 487451

=======

MGOGORO NAMANGA: Hali ya Taharuki leo imelikumba eneo la Namanga ulipo Mpaka wa Tanzaniana Kenye Baada ya wananchi Wakenya kufunga eneo huru la Nomad Land na kuzuia magari yaliyokuwa yanatoka Tanzania kuingia kenya wakishinikiza kuachiwa wenzao waliokamatwa kwa madai ya kuishi upande wa Tanzania Bila Kibali.

Hata hivyo Viongozi wa eneo hilo waliingilia kati na kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya Longido Daniel Chongolo amesema wamefikia makubaliano kumaliza mgogoro kwa kufuata Sheria hivyo wanaotaka kuishi Tanzania lazima wafuate taratibu sawa na watanzania wanaotaka kuishi upande wa Kenya.

Chanzo: Mwananchi

--------------------
Habari kutoka KENYA

View attachment 487573

Kenyans in Namanga demonstrated against Tanzanian leader John Magufuli on Monday saying he had deported their counterparts.

They paralysed transport by blocking the Kenya-Tanzania border road at Namanga and stormed businesses owned by Tanzanians.

They rounded the foreigners up and frog-marched them across the border to their country. Many from Magufuli's country claimed they lost their stock and money.

Tanzanian barmaids working in Kenyan clubs were roughed up and their mobile phones taken away.

Businesses on the Kenyan side remained closed until after midday.

The Star reported in January that Tanzanian authorities were targeting Kenyans living in their country illegally.

Several Kenyans, including those who were born in Tanzania before independence, have been told to leave if they cannot provide documents validating their stay.

Others were born by Kenyan parents living in Tanzania in the early 1960s and have no other links.

Samuel Ngeselai was forced to flee Longido district in Tanzania and move to Kenya, leaving his children and wife of 30 years across the border. He is now stateless.

Ngeselai said his grandfather, a Mau Mau activist who escaped to Tanzania early in the 1950, died there.

His mother is bedridden and still living in Tanzania.

Kajiado county commissioner Harsama Kello said the demonstrations began at the border after Tanzanian authorities arrested three Kenyans last Friday and arraigned for being in the country illegally.

“Countries carry out routine checks. Our people should respect the law and ensure they have valid immigration documents while in foreign countries,” Kello said.

The commissioner said a contingent of security personnel was sent to the border to end the protests. He said two weeks ago that the situation was under control.

As Kello addressed journalists, a group of Kenyans was seen destroying Kenya Power transformers to cut off the link with Tanzania. Police watched as they vandalised the transformers.

He added that top officials from the immigration department and local police officers were in a closed-door meeting in Namanga on restoring normalcy.

The Tanzanian High Commission in Nairobi denied that Operation Timua Wageni is a move to free up jobs for locals.

The High Commission told the Star that the exercise that began in January is routine enforcement of the Tanzanian Immigration Act of 1995 and does not target any nationality.

“What I can tell you is that this is not something new. It has always been there,” said an official who did not want to be identified because of lacking authority to speak to the press.

The Tanzanian government launched a crackdown on foreign nationals who do not have both work and residence permits.

Only 680 foreigners have work permits, according to the country's immigration department, while only 66 have applied for residence permits.

Source: Kenyans protest Magufuli order to deport foreigners, block Namanga border
DRUNCARDS THINK THEY CAN GO AGAINST THE LAW AND LIVE IN OUR COUNTRY !
 
Rais anashinda kwenye mitandao ila hataki wengine watumie mitandao ya kijamii roho mbaya haijawaki kutokea.
wengine wafanye kazi yeye kutumbua na kuteua hiyo nayo kazi?
tehe tehe tehe kabisa, asitupangie
 
Yule
Omba sana na ushukru RC Bashite hayuko kwenye mkoa wa mpakani! Huyu anaweza kusababisha Vita baina ya Tanzania na Kenya kwa akili zake za divisheni sifuri!!!!!!llj
Kijana Ana haraka Sana , utulivu nehi
 
Kama wanakaa hapo kinyume na sheria watimuliwe kama waTZ tulivyofanyiwa msumbiji na isiishie hapo iwe operation ya nchi nzima.
Hongera Mh. Lazima tufuate sheria. Kama Mchumbiji sawa kwanini isiwe Kenya. Wafunge, hasara ni kwao.
 
Sasa, umesema ni wakenya wanaoishi Tanzania eneo.la.mpakani sasa, hao si ni wahamiaji haramu

Mpaka acha ufungwe tu!!
Asante Mkuu. Tuna unga mkono juhudi na uzalendo mkubwa sana wa Mh. Magufuli.

Humu wauza unga wanampinga kwa kila jambo.
 
Back
Top Bottom