Arusha: Mmiliki wa Madrasa adaiwa kulawiti wanafunzi 22

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,738
15,211
Mkuu wa wilaya ya Arusha ameingilia kati sakata la mmiliki wa madrasa kulawiti watoto 22 ambao ni wanafunzi kwenye madrasa yake kwani imeonekana analindwa na kukingiwa kifua na baadhi ya vigogo wa rushwa ili kuzima swala hilo.

--
Mwalimu wa madrasa, Jumanne Ikungi anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani wa Arusha kwa tuhuma za kuwalawiti wanafunzi zaidi ya 20 wa shule ya msingi Mkonoo katika jiji la Arusha.

Tukio hili la aina yake limeibuliwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Said Mtanda leo Mei 18 baada ya kufika katika shule hiyo na kuzungumza na wazazi, walimu na wanafunzi baada ya kukamilisha alichoita uchunguzi wake juu ya mwalimu huyo wa madrasa.

Amesema Mwalimu huyo wa madrasa amekuwa akiwarubuni Kwa pipi miwa na zawadi nyingine watoto hao na kuwafanyia ukatili ambao Serikali haiwezi kuvumilia.

"Nimeagiza wanafunzi waendelee kufanyiwa uchunguzi katika hospitali na madrasa kufungwa na kuendelea kishikiliwa na polisi mtuhumiwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika," amesema.

Mtanda katika shule hiyo iliyopo pembezoni mwa jiji la Arusha ameagiza wanafunzi wote kuandika upya kama wamefanyiwa matukio yoyote ya ukatili na baadae Serikali itafanya uchunguzi zaidi.

Mkuu huyo wa wilaya ametaka wazazi katika jiji la Arusha kuwa karibu na watoto wao na kuwafanyia uchunguzi mara Kwa mara hasa kutokana na kuongezeka matukio ya ukatili.

"Abiria chunga mzigo wako, sasa wazazi wachunguzeni watoto katika wilaya ya Arusha tuna shule 49 zote tunatoa chakula Cha mchana sasa kuwaona watoto mtaani ni jambo ambalo halikubaliki," amesema.

Awali Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mkonoo, Lucian Monino amesema walianza Kubaini uwepo wa matukio ya uhalifu baina ya wanafunzi na Mzee Jumanne anayeishi jirani na shule baada ya utoro kuongezeka shuleni.

"Baada ya utoro tulianza uchunguzi na tulibaini Kuna wanafunzi wengi wanaishia kwa mzee Jumanne kufanyiwa ukatili.

"Tuliwahoji na walikiri baadhi kufanyiwa ukatili wanapokwenda madrasa na kwenye nyumba ya mzee huyo ambaye anaishi peke yake," amesema.

Jeshi la polisi mkoa Arusha limekiri kumshikilia Jumanne Ikungi na uchunguzi ukikamilika atafikishwa Mahakamani.


Chanzo: Mwananchi

 
Ndugu jumanne alikua akiwapatia watoto wale soda, pipi na miwa, alikua akiwaangiza kwenye chumba cha mafunzo kisha kuwavua nguo halafu akiwaamuru walalie matumbo huku yeye akipaka mafuta na kuwashughulikia baadae akiwapatia zawadi kama soda, pipi na miwa.
 
Back
Top Bottom