Arusha: Madiwani Watatu wa CHADEMA wahamia CCM

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,609
Reaction score
62,371
ZIARA ya kwanza ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Lootha Sanare katika Wilaya ya Ngorongoro, imeanza kwa kimbunga na kuvunja ngome ya Chadema baada ya madiwani watatu wa chama hicho kujiengua na kuhamia chama tawala.

Sanare ameanza ziara juzi ya kutembelea wilaya zote saba za Mkoa wa Arusha kuangalia uhai wa chama na kuangalia kama ahadi za madiwani wa CCM kama zimeanza kutekelezwa pale walipoomba ridhaa ya kutaka kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Katika ziara hiyo iliyoanza katika Tarafa ya Ngorongoro, ilianza kwa madiwani hao watatu kujiengua Chadema katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ngorongoro kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, William Ole Nasha.

Madiwani waliojiengua Chadema na kuhamia CCM kwa ridhaa yao ni Diwani wa Kata ya Ngorongoro, Daniel Orkeriy, Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Wilaya hiyo na pia Diwani wa Kata ya Ngoile, Lazaro Saitoti na Diwani wa Kata ya Loitole, Sokoine Moiv.

Viongozi hao walisema kujiengua kwao kumetokana na kukengeuka na kujikuta wakiwa Chadema bila kutafakari na uamuzi huo umewaathiri katika utendaji wao na kurudi kuijenga CCM na kuwa kitu kimoja kwa maslahi ya nchi.

Pili walisema uamuzi waliochukua ni utashi wao na siyo kushawishiwa kwa namna yoyote bali ni kuona yale waliyokuwa wakitaka kuyafanya sasa yanafanywa kwa kasi ya hali ya juu na Rais John Magufuli, hivyo kumewafanya kushawishika kurudi nyumbani baada ya kupotea mbugani kwa kufuata mkumbo.

Akizungumzia uamuzi huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Sanare alisema ziara yake imeanza kwa mafanikio na kuongeza kuwa wakati wa kuizika Chadema wilayani Ngorongoro na Mkoa wa Arusha kwa ujumla umefika na kuwataka wana CCM kuwafungulia mlango wale wote waliopotea kurudi nyumbani kujenga nchi.

Aliwataka walioamua kung’ang’ania Chadema kama kupe kujitafakari na kuchukua uamuzi kuikubali kazi ya Rais Magufuli na kurudi CCM kwani kwa kufanya hivyo hakutakuwa kwa ajabu, bali uamuzi wa kijasiri.

Alisema mgombea wa Urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa alikwenda Ikulu na kumsifu Rais Magufuli kwa kazi nzuri ya kujenga, na kuwataka wengine wenye roho ngumu kufanya hivyo kwani siyo dhambi. “Tufungue milango wanaCCM wenzangu na kuwapokea kwa mikono miwili wale waliokengeuka na kwenda Chadema kwani wameshakubali kuwa mziki wa Rais Magufuli siyo muziki wa kawaida,” alisema Sanare.

Mbunge wa jimbo hilo, Ole Nasha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, aliwashukuru madiwani hao kwa uamuzi huo na kuwakaribisha kufanya kazi yenye lengo la kukijenga chama katika wilaya hiyo.
 
Na hawa tumewachoka,
Hawahawa ndio wanaotusababishia vifo
 
Magufuli anataka kutawala milele kwa hii style atauwa upinzani then ataweka mapandikizi yake yatakayo kuwa yanamuunga mkono.

Another Uganda cming soon
 
Duh hivi hii nchi ya ajabu kiasi gani? Hivi kushinda kutwa kucha jitu linasema nimeamua kwanini uligombea ?? Mijitu ya aiana gani hii inatuongezea gharama kila uchao?
 
Hakuna kinacho nikera kama story kma hizi, hlf kujiuzuru gao viongozi watatu hakuna faida siku zote bora ije habari kuwa wanachana 300, wamejiunga na chama fulan make hizo ni kura za ku make a big diffrrence, siku hizi mtu akihama watu wamekuwa wajanja, wanamwacha ahame mwenyewe make kma ni hela kavuta mwenyewe.
 
Duh hivi hii nchi ya ajabu kiasi gani? Hivi kushinda kutwa kucha jitu linasema nimeamua kwanini uligombea ?? Mijitu ya aiana gani hii inatuongezea gharama kila uchao?
Kwanini mliwasimamisha?
 
One of the guys ni rafiki yangu, alikula pesa za wananchi milioni 30, alibanwa mbavu na sasa plan iliyoaki ni kuhamia ccm ili afutiwe kesi. You could have done the same bro. Mwingine ni schoolmate wangu, alikuwa na kesi mahakamani ya kuchana bendera ya ccm kipindi cha uchaguzi na kesi ilikuwa mahakamani, naye kamwaga pesa za kutosha maana kesi inazungushwa mno na yupo karibu kufilisiwa kabisa. The last man naye alitumia vibaya pesa za mradi wa kuchimba maji uliofadhiliwa na kanisa katoliki ikishirikiana na serikali.All in all hawa jamaa makosa yao ndo yametumika kama silaha ya kuwaangamiza na kusalitishwa chama. Ni wakosaji wangetakiwa kuwa ndani ila ndo hivo tena, kuhamia ccm means makosa yako yamefutika.
 
Hata Mimi hakuna story inayonikera kama kusikia huyu viongozi wakuchaguliwa na umma kuhamahama vyama na kusababisha CHAGUZI.

ingekuwa Mimi na Uwezo wa kimiujiza ningemfanya SALIM MWALIMU mgombea wa CHADEMA Kinondoni awe Mshindi halafu baada ya kuapishwa Kyle DODOMA atangaze Kujiuzulu Ubunge.

Kisha turudie UCHAGUZI na CHADEMA wamteuwe yy huyohuyo kugombea tena na Mtindo uwe huo huo yawezekana viongozi wetu ndo watastuka na kuona kuwa.

Kuondoa wafanyakazi hewa au waliofoji vyeti ! Au kupambana na ufisadi wa RUSHWA au, kupambana na wezi wa Madini/makinikia au kuzuia Semina na warsha na elimu zingine za uelekezi kwa wafanyakazi au kuzuia safari za nje zisizo za lazima kwa watumishi.

Kisha kumwaga fedha kwenye chaguzi za marudio zisizona sababu ni FEDHEHA kama Taifa yaani HATUJITAMBUI yaani siasa ni sifa kuliko UTAIFA.

Mgombea akijiuzulu eneo la kiutawala likae wazi hakuna kinachoharibika , nenda maeneo yote na Yale ambayo chaguzi hazijarudiwa kote matatizo kwenye Huduma za wananchi yapo huku fedha zikitumika kwenye ufahari wa kisiasa.

Nenda Kinondoni Leo, barabara mbayaaaa, Shule za msingi na kata ni za hovyoooo, muundo mbinu haifaiii, masoko machafuuuu, vituo vya daladala hovyoooo nk

Leo wanatapanya fedha kwa fahari ya kijinga ya KISIASA.

MBONA HIZI NI SIASA ZA HOVYO NANI KATULOGA NI KENYA, UGANDA, MALAWI ,AU ZIMBABWEE,

Hapana hili ni gonjwa la akili.

Kweli MTU makini kwa matumizi ya fedha kama JPM halioni hili, au kina HUMPHREY wanataka wamuoneshe Mkuu wanachapa kazi.

Hapana wanasiasa ni wachache wawaheshimu WATANZANIA.
 
Hizi sanaa tu, tumemaliza Jana kampeni za udiwani na ubunge wa marudio katika majimbo ya Kinondoni na Siha lakini hatujaona wananchi wakijiunga ccm zaidi ya hawa viongozi waliohongwa, hivyo ni uthibitisho ulio wazi kabisa wananchi hawajaona la maana kwenye serikali ya awamu hii ya JPM
 
Acha waende sisi tunaangalia wapiga kura atuangalii madiwani wa3
 
ZIARA ya kwanza ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Lootha Sanare katika Wilaya ya Ngorongoro, imeanza kwa kimbunga na kuvunja ngome ya Chadema baada ya madiwani watatu wa chama hicho kujiengua na kuhamia chama tawala.

Sanare ameanza ziara juzi ya kutembelea wilaya zote saba za Mkoa wa Arusha kuangalia uhai wa chama na kuangalia kama ahadi za madiwani wa CCM kama zimeanza kutekelezwa pale walipoomba ridhaa ya kutaka kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Katika ziara hiyo iliyoanza katika Tarafa ya Ngorongoro, ilianza kwa madiwani hao watatu kujiengua Chadema katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ngorongoro kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, William Ole Nasha.

Madiwani waliojiengua Chadema na kuhamia CCM kwa ridhaa yao ni Diwani wa Kata ya Ngorongoro, Daniel Orkeriy, Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Wilaya hiyo na pia Diwani wa Kata ya Ngoile, Lazaro Saitoti na Diwani wa Kata ya Loitole, Sokoine Moiv.

Viongozi hao walisema kujiengua kwao kumetokana na kukengeuka na kujikuta wakiwa Chadema bila kutafakari na uamuzi huo umewaathiri katika utendaji wao na kurudi kuijenga CCM na kuwa kitu kimoja kwa maslahi ya nchi.

Pili walisema uamuzi waliochukua ni utashi wao na siyo kushawishiwa kwa namna yoyote bali ni kuona yale waliyokuwa wakitaka kuyafanya sasa yanafanywa kwa kasi ya hali ya juu na Rais John Magufuli, hivyo kumewafanya kushawishika kurudi nyumbani baada ya kupotea mbugani kwa kufuata mkumbo.

Akizungumzia uamuzi huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Sanare alisema ziara yake imeanza kwa mafanikio na kuongeza kuwa wakati wa kuizika Chadema wilayani Ngorongoro na Mkoa wa Arusha kwa ujumla umefika na kuwataka wana CCM kuwafungulia mlango wale wote waliopotea kurudi nyumbani kujenga nchi.

Aliwataka walioamua kung’ang’ania Chadema kama kupe kujitafakari na kuchukua uamuzi kuikubali kazi ya Rais Magufuli na kurudi CCM kwani kwa kufanya hivyo hakutakuwa kwa ajabu, bali uamuzi wa kijasiri.

Alisema mgombea wa Urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa alikwenda Ikulu na kumsifu Rais Magufuli kwa kazi nzuri ya kujenga, na kuwataka wengine wenye roho ngumu kufanya hivyo kwani siyo dhambi. “Tufungue milango wanaCCM wenzangu na kuwapokea kwa mikono miwili wale waliokengeuka na kwenda Chadema kwani wameshakubali kuwa mziki wa Rais Magufuli siyo muziki wa kawaida,” alisema Sanare.

Mbunge wa jimbo hilo, Ole Nasha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, aliwashukuru madiwani hao kwa uamuzi huo na kuwakaribisha kufanya kazi yenye lengo la kukijenga chama katika wilaya hiyo.
Ifike wakati sasa tuone uchungu kwa pesa za walipa kodi. Wanakotoka na wanakokwenda, chonde chonde wajitathimini kuwapokea hawa wahaini.
 
Back
Top Bottom