Arusha, Kilimanjaro : Kila wiki Kuna ongezeko jipya la Pombe Feki tishio Kwa nguvu kazi iliyobakia

Arusha, Kilimanjaro : Kila wiki Kuna ongezeko jipya la Pombe Feki tishio Kwa nguvu kazi iliyobakia

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
10,414
Reaction score
18,438
Ukweli ni kwamba Kuna ongezeko la kutisha za pombe aina mbali mbali za makopo pamoja na zile za kupima ambazo hazina viwango.

Kutokana na ugumu wa maisha makundi yote nikimaamisha vijana Kwa wazee, wanawawake na mabinti wengi wamekuwa watumiaji wazuri wa hizo pombe huku wakilalamika aina ya ladha na ukali wa hizo pombe kuwa ipo siku zitawaua.

Wengi wa wanywaji hao wanakimbilia hizo pombe kutokana nakuuzwa bei rahisi pamoja na kuwa na kiwango kikubwa Cha kilevi.

Pombe ya "buku "mtu anaelewa na harakati zinaendelea kama kufa acha tufe TU kwani nani ataishi milele aisee, mmoja wa wanywaji akieleza kwanini anakunywa aina hiyo ya pombe.

Maduka ya chakula Almaarufu Kwa Mangi wamekuwa pia wauzaji wa Kila aina za pombe hizo na huku wakidai kuwa Kila wiki Kuna toleo jipya za pombe za makopo.
 
Back
Top Bottom