Arusha: Kampuni ya Sinohydro idhibitiwe

Arusha: Kampuni ya Sinohydro idhibitiwe

Kichumi

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
588
Reaction score
515
Kampuni ya Sino hydro inajenga mradi wa maji taka jijini Arusha pamoja na maeneo ya jirani. Hata hivyo kampuni hii imekuwa kero kubwa kwa wakaazi wa Arusha kwa kuharibu miundombinu ya barabara za mitaani na mifumo mitaro ya maji ya mvua.

Baadhi ya maeneo kama Njiro kuna mitaa haipitiki kabisa kwa miguu na magari sababu ya uharibifu uliofanywa na kampuni hii.

Wananchi wamelalamikia viongozi wa kampuni hii lakini hakuna kinachofanyika zaidi ya wao kujibu wao wana mkataba wa kujenga mfumo wa majitaka peke yake, uharibifu wanaoufanya wanaacha hivyo hivyo.

Tunaomba Serikali ya Mkoa wa Arusha iingilie kati kwani madhila wanayopata watu wa Arusha kwa kero zinazosababiswha na kampuni hii zimezidi.

Ni matumaini yetu kuwa Serikali itasikiliza kilio cha wananchi wa Arusha.
 
Kampuni ya Sino hydro inajenga mradi wa maji taka jijini Arusha pamoja na maeneo ya jirani. Hata hivyo kampuni hii imekuwa kero kubwa kwa wakaazi wa Arusha kwa kuharibu miundombinu ya barabara za mitaani na mifumo ya maji ya mvua.

Baadhi ya maeneo kama Njiro kuna mitaa haipitiki kabisa kwa miguu na magari sababu ya uharibifu uliofanywa na kampuni hii.

Wananchi wamelalamikia viongozi wa kampuni hii lakini hakuna kinachofanyika zaidi ya wao kujibu wao wana mkataba wa kujenga mfumo wa majitaka peke yake, uhaibifu wanaoufanya wanaacha hivyo hivyo.

Tunaomba Serikali ya Mkoa wa Arusha iingilie kati kwani madhila wanayopata watu wa Arusha kwa kero zinazosababiswha na kampuni hii zimezidi.

Ni matumaini yetu kuwa Serikali itasikiliza kilio cha wananchi wa Arusha.
Kweli barabara za njiro hazipitiki haswa mitaa ya tanesco,lemara,nanenane wanapita wenye 4×4 tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom