Dr, anastahili kuheshimiwa kwani amejipambanua kuwa mkweli na mchambuzi makini katika masuala yanayogusa jamii/walio wengi. Hataki kuonyesha unafiki katika masuala yanayojieleza. Muda mwingi nimekuwa nikimfuatilia na kugundua kuwa anachukia sana uonevu bila kujali unafanywa na nani. Nimependezwa na dhana ya kuwa na vyama viwili vikubwa vyenye nguvu ambavyo vinaweza kushindana na yeyote akashinda kwa nguvu za hoja badala ya kuwa na utitiri wa vyana kibao, ambavyo vingine vinaweza kutumika kama wasindikizaji katika siasa. Big up Dr. endelea kuwa hivyo