Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Afisa usalama wa wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha,Issa Selfu Ng’itu amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Arumeru na kuunganishwa kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uwindaji ya Otterlo Business Corporation(OBC) , Isack Mollel(59) na kusomewa makosa 15 ya rushwa ,kuwasilisha nyaraka za uongo na kughushi.
Akisomewa mashitaka hayo na Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Serikali, Osward Tibabyekomya akisaidiwa na mwanasheria mkuu wa serikali mkoani hapa, Materius Marandu mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Arumeru, Obadia Bwigwegwe ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo kati ya mwaka 2014 hadi 2019 katika maeneo tofauti wilayani Ngorongoro,jijini Arusha na jijini Dar es salaam.
Tibabyekomya alidai kuwa shitaka la kwanza linalomkabili Ng’itu mnamo Juni 20, 2016 katika eneo lisilojulikana wilayani ngorongoro alijipatia kiasi cha shilingi milioni 1 kutoka kwa mkurugenzi wa OBC isaya Mollel wakati akijua ni kinyume cha sheria.
Shitaka la pili mnamo septemba,2mwaka 2016 afisa huyo wa usalam,a alijipatia manufaa ya sh, milioni 1 kutoka kwa mkurugenzi wa Isaya Molle ambaye ni mkurugenzi wa OBC kinyume cha sheria
Shitaka la tatu mnamo septembe 2,2016 katika eneo la ngorongoro ,Ng’itu alijipatia manufaa y ash,milioni 1 kutoka kwa Isaya Mollel mkurugenzi wa OBC KUNYUME CHA SHERIA.
Shitaka la nne mnamo septembe 9,2016 katika eneo la ngorongoro Ng’itu alijipatia kiasi cha sh, milioni 1 kutoka kwa Isaya Mollel mkurugenzi wa OBC kinyume cha sheria.
Mwendesha mashitaka akisoma shitaka la tano alidai kuwa mnamo desemba 2mwaka 2016 katika eneo la ngorongoro ,Ng’itu alijipatia kiasi cha sh,milioni 1 kutoka kwa Isaya Mollel Mkurugenzi wa OBC kinyuem cha sheria.
Shitaka la sita mnamo januari 13, 2017 katika eneo la Ngorongoro,Ng’itu alijipatia manufaa ya shilingi milioni 1 kutoka kwa Mollel mkurugenzi wa kampuni ya OBC ,Kinyume cha sheria.
Alisoma shitaka la saba mnamo januari 14,2017 katika eneo la ngorongoro ,Ng’itu alijipatia kiasi cha sh,5500 kutoka kwa Mollel mkurugenzi wa kampuni ya OBC kinyume cha sheria.
Mwendesha mashitaka wa serikali alisoma shitaka la nane alidai kuwa mnamo januari 14,2017 katika eneo la ngorongoro Ng’itu alijipatia manufaa ya sh, milioni 1 kutoka kwa Isaya Mollel Mkurugenzi wa kampuni ya uwindaji ya OBC, wakati akijua ni kinyume cha sheria.
Tibabyemkomya alisoma shitaka la tisa alidai kuwa mnano januari 25,2017 katika eneo la ngorongoro Ng’itu akiwa ofisa usalama alijipatia manufaa ya sh, milioni 1 kutoka kwa Isaya Mollel mkurugenzi wa OBC KINYUME CHA SHERIA.
Shitaka la kumi mnamo januari 26 ,2017 katika eneo la ngorongoro, Ng’itu alijipatia kiasi cha sh,milioni 1 kutoka kwa isaya Mollel mkurugenzi wa OBC, kinyume cha sheria.
Akisoma shtaka la 11,Tibabyenkomya alidai kuwa kati ya tarehe 11 hadi 14 Ng’itu alijipatia gari aina ya Land Cruser Prado lenye namba T 456 DFZ kutoka kwa isaya Mollel kinyume cha sheria.
Shtaka la 12 linawakabili washtakiwa wote wawili, Issa Ng’itu na Isaya Mollel ambapo kwa pamoja mnano Mach 14,2014 katika jiji la Dar es salaam wakiwa na nia ya kudanganya walighushi nyaraka na kubadilisha mkataba wa gari aina ya Prado na kuonyesha liliuzwa kiasi cha sh, milioni 2.
Shtaka la13 ni mshitakiwa wa pili Isaya Mollel, ambapo mnano tarehe 14,mach,2017 aliwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka ya mapato TRA wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam kuuziana gari aina ya Prado lenye namba T 456 bfz kwa kiasi cha sh,milioni 2.
Shtaka la 14 ni la mshtakiwa namba moja Isa Ng’itu mnamo julai 15,2017 alipokea kiasi cha sh,milioni 1 kutoka kwa isaya Mollel wakati akijua ni kinyuem cha sheria.
Katika shtaka la 15 linawakabili washtakiwa wote wawili mnamo februali 18 ,2019 jijini Arusha walighushi nyaraka ya tarehe 11,machi 2017 na kuonyesha wameuziana gari aina ya Landcruser namba T 456 bfz kiasi cha shilingi milioni 27 jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Hakimu Bwigwegwe aliahirisha kesi hiyo April 11,mwaka huu huku washtakiwa wakienda rumande kutokana na kosa lao kutokuwa na dhamana kisheria.
Washtakiwa ambao hawakutakiwa kujibu chochote walikuwa wakiwakilishwa na wakili Adiel Abrahamu na Daud Haraka.