VoiceOfReason
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,194
- 1,375
Point yangu ni kwamba Arsenal haina uwezo wa kununua wachezaji kama United haina hizo pesa..., United amekuwa akitumia pesa nyingi lakini Arsenal amekuwa akitumia kiasi kidogo cha pesa.., kwa matumizi mazuri ya pesa hadi Arsenal iliweza kujenga uwanja wa Emirates.., Kwahiyo kwa usajili mbovu wa Sir Alex au uwezo mdogo wa kupata undiscovered talent kwahiyo ingekuwa vigumu kwa Sir Alex kumage aliyoweza Wenger Arsenal, Wenger anawapenda wachezaji wa France sababu ndipo alipotoka ni rahisi kuwaelewa kuliko wengine, Kipindi Gilberto yupo mwisho wa siku alikuwa anafunikwa na Flamini.., angekuwa bado mtaalamu asiingeenda OlimpiacosUwezo wa Wenger hamfikii kabisa Ferguson labda kwenye mambo mengine na sio football
Manchester United wanatumia fedha kununulia wachezaji kwa sababu ya umuhimu ya wachezaji wanaowahitaji na kiasi cha pesa unacho .Kweli kuna wachezaji wamenunuliwa kwa pesa nyingi lakini wengi wao wameleta faida kwenye klabu wachezaji kama Ruud Van Nistelrooy,Rooney,Ferdinand pamoja na kununulkiwa kwa fedha nyingi thamani yao inaonekana.Umesahau kuwa kuna wachezaji ambao Fergie kawnunua kwa bei chee na wameonyesha uwezo mkubwa Vidic,Evra,Park,Chicharito,Ronaldo,Van de Sar wamenunuliwa kwa bei chee lakini uwezo wao unaonekana.
Suala la kukorofishana na wachezaji hiki ni kitu cha kawaida kwa binadamu ,kila mtu ana msimamo wake hata Guardiola alipopewa ukocha Barca alisema wazi hana mpango na Ronaldinho,Etoo lakini still Barca inafanya vizuri.Juzi Denilson na Bertnder wamemlaumu Wenger,pia sijakusikia kwa nini hujazungumzia suala la Wenger kuwapendelea wachezaji wa kifaransa au kwa nini alimnyima Gilberto ukapteni akampa Gallas,then kwa nini Gallas akaondoka Arsenal.
1. anapenda wachezaji wa France sababu ndipo lipotoka hence anawaelewa vizuri kuliko wachezaji wa nchi nyingineMatatizo ya Arsene Wenger
- Anapenda sana wachezaji wa kutoka France(Wafaransa au kutoka Ligue1) wengine hawastahili kuchezea Arsenal,mfano Diaby,Squilaci,Koscielny
- Anashindwa kujenga timu ya muda mrefu,kuna kikosi alianza kukijenga kikiwa na kina Fabregas,Sagna,Clich,Gallas,Toure,Adebayor,Hleb,Flamini lakini kwa uzembe wake wachezaji wengi waliondoka akaanza tena kujenga timu sasa Fabregas,Clichy,Nasri,Denilson,Bertnder nao wanataka kuondoka.Kuna wachezaji anakuwa na uwezo wa kuwazuia wasiondoke kwa kuwaongezea mishahara au njia nyingine
- Kuna wachezaji wengi walikuwa wazuri kwenye timu zao but walipofika Arsenal viwango vyao vinaanza kuporomoka mfano Rosisky,Arshavin,Chamakh
- Ni mbishi kufanya maamuzi ingawa kuna matatizo ya wazi yanaonekana waziwazi baada ya kuumia Vermalen watu walitarajia atanunua replacement hakununua tukafikiri labda Januari nayo hakununua
- Hataki kuwapa nafasi wachezaji wazawa,tumeona backbone ya Barca ni wachezaji kutoka Spain,AC Milan wapo kina Gatusso but tangu wameondoka kina Tony Adams timu haina wachezaji wazawa ambao mara nyingi wanakuwa na uchungu kuliko wageni.Kwa mtazamo wangu Ashley Cole ni mchezaji ambae hakupaswa kuondoka Arsenal na huenda leo angekuwa nahodha labda angekuwa anawafokea kiana Diaby,Fabregas na wengine
1. anapenda wachezaji wa France sababu ndipo lipotoka hence anawaelewa vizuri kuliko wachezaji wa nchi nyingine
2. Wachezaji hawaondoki kwa uzembe wake bali sababu wanalipwa pesa ndogo wanataka waende pengine walipwe nyingi ila wachezaji wote wanapoondoka Arsenal huwa wanakuwa flops, Henry, Viera, Pires, Hleb to name just a few
3.Wachezaji inategemea na mfumo wa timu, Wenger alibadilisha mfuno wa Arsenal Kucheza kama Bolton na kuwafanya wacheze kama Barcelona
4. Kununua wachezaji sio suluhusho la kupata kombe muulize Man City; pia kupata mchezaji anayefaa sio lele mama muulize Ferguson ni makosa mangapi amefanya
5. Wachezaji wa England ni expensive na overhyped, 16m kwa michael carrick, 12 kwa Crouch na 30m kwa Rio Ferdinand.., kwahiyo kununua England ni overpriced goods
Yaani in short kwa pesa United ambazo wametumia na wanapata kwa miaka zaidi ya 20 kushinda Champions league mbili ni kwamba wameflop kulinganisha na returns, hayo majina yote unayoyataja hao wote wachezaji walikuwa wanajulikana ndio sababu anaspend pesa nyingi kuwachukua, tofauti na Arsenal analeta watu wasiojulikana hence kutumia pesa kidogo ni sawasawa na kama una pesa za kununua Ferrari wewe unanunua pijo...., Sir Alex amekuwa na pesa nyingi sana za kutumia kila akitaka tofauti na WengerNazungumzia kutumia fedha kiasi kidogo na kuleta mafanikio yanayoonekana kwa misimu 6 iliyopita sawa ametumia kiasi kidogo but ameleta mafanikio gani?
Uwanja wa Emirates hilo linajulikana ni fedha za mkopo kutoka Shirika la ndege la Emirates na Arsenal wanalipa deni kidogo kidogo hadi watakapomaliza.Sidhani kama angekuwa na uwezo mdogo wa kusajili angeweza kuwasajili wachezaji kama Evra,Vidic,Ronaldo,Chicharito,Rafael & Fabio.Kwa sasa ukiangalia pia SAF tayari ana timu ya misimu 5 ijayo yenye vijana kama Rafael,Fabio,Jones,Smalling,Chicharito,Pogba,Anderson,Nani,Valencia
- Sawa ni rahisi kuwaelewa but wengi wao viwango vyao ni vibovu hawastahili kuchezea Arsenal. Diaby,Squilaci,Koscielny hawa hawafai kuchezea Arsenal hata kama wanatoka Brazil.
- Wachezaji kama Flamini & Cole Wenger alikuwa anaweza kuwazuia issue ilikuwa kuongeza mshahara ambao Wenger anaweza akaishawishi bodi kutokana na umuhimu wa wachezaji.Kuhusu kuwa flop Henry,Pires& Viera waliondoka wakiwa tayari viwango vyao vimeanza kushuka,wengine kina Hleb,Henry,Flamini walikuwa flop kutokana na kwenye kwenye ligi nyingine zenye mifumo tofauti angalia viwango vya Toure,ACole,Gallas,Upson ambao wamebaki EPL.
- Barcelona wanacheza mopira mzuri na wanashinda ,while Arsenal wanajaribu kucheza mpira mzuri na wanafungwa hiyo ndio tofauti
- Sawa kununua wachezaji sio kupata makombe but kuna kuna pengo linaonekana linatakiwa lizibwe,baada ya kuumia Vermalen hakuna beki ambae aliweza kuziba pengo lake
- Kweli wachezaji wa kiingereza ni bei ghali but ili uweze kushindana kwenye ligi ya nyumbani lazima uwe na wazawa,nimekupa mifano ya Barca,Milan,Bayern,Manu,Chelsea zote zina wachezaji wazawa ambao pamoja na kuwa wengine wana viwango vibovu but wanahimili mikikimikiki ya ligi,na sidhani kama Aston Villa wanaweza kumsajili Daren Bent halafu Arsenal washindwe kumsajili Scott Parker au Gary Cahill
Kwa England kazi ya manager ni kununua wachezaji pia na sio kufundisha tu mpira; sasa basi tukija kwa Ferguson:Nafikiri title ya thread yako ingekuwa Wenger anajua kutumia fedha vizuri kuliko Ferguson
Taja wachezaji alionunua Wenger na SAF na taja waliofanya vizuri na walioflop tulinganisheKwa England kazi ya manager ni kununua wachezaji pia na sio kufundisha tu mpira; sasa basi tukija kwa Ferguson:
Veron, Taibi, Djemba Djemba, Michael Carrick, Owen (kwa pesa alizotumia); Swali linakuja kwamba huenda usajili sio strong point ya Sir Alex; na kama unatimu ambayo haiwezi kumwaga pesa za kupoteza Sir Alex is not your Man; Na labda kina Bergamp Scholes Neville wote wasingetokea Academy maybe huyu jamaa anageflop.
wenger ni sawa na mkia wa Mbuzi...haustiri uchi wala haufukuzi Nzi.
Ktk makocha vilaza niliopata kuwaona Wenger ndie kinara wa Vilaza.
Hebu jiulize tangu timu imepata uwanja mpya na kuwa na pesa je ina mafanikio gani?
well mtoa mada anajaribu kusema eti kwa kubadili mfumo toka 4-5-1 mpaka 4-4-2 basi Arsenal ilianza kucheza mchezo wa kuvutia mpaka washabiki wakarudi tena na kumiminika uwanjani...
Sasa mi najiuliza ni bora ya 4-5-1 ambayo soka lilikuwa bovu lakini mafanikio ya vikombe yanaonekana au 4-4-2 ambayo hakuna kimombe wala bilauli?
mkumbuke jamani kuwa mafanikio ya timu sio pesa.
Mafanikio ya timu ni Vikombe.
Naomba kuwasilisha hoja.
WengerTaja wachezaji alionunua Wenger na SAF na taja waliofanya vizuri na walioflop tulinganishe
ndugu muanzisha thread nadhani hizi link zitakusaidia Alex Ferguson - Wikipedia, the free encyclopedia Arsène Wenger - Wikipedia, the free encyclopedia
labda kama unazumgumzia mafanikio kwa muda ambao makocha hao wamefanya kazi uingereza peke yake.
Ferguson ameweza kuibadilisha Man U kuwa timu tajiri zaidi duniani na kuwa na mashabiki wengi.
Upande wa kusajili, unapaswa kujua yeye ni manager, kuna scouts ambao kazi yao ni kutafuta wachezaji na kumshauri yupi wa kumnunua.
Katika timu ya Man U, unaweza kuona 'age layers' kwenye kikosi cha kwanza; layer ya kwanza Rio, Giggs, Gary, Scholes etc, layer nyingine Rooney, Fletcher, Nani, Gibson etc na nyingine Welbek, Da silvas, De laet, Jones. Hiki ni kitu ambacho Ferguson ameweza kumaintain kwa muda mrefu akiwa manager, Wenger ameshindwa kabisa.
Kitu alichokifanya Ferguson kuchukua kombe scotland ni kama vile Benitez alivyochukua kombe Spain naMkuu kazi ya manager England ni kusajili pia yeye ndio anakuwa na Last say sio kama spain na mafanikio ndio tunaangalia kwenye Big leagues sio Scotland alikotoka Alex au Japan alipokuwa Wenger.
Man United ilikuwa tajiri na following yake ilikuwa kubwa, mkuu tangia zamani hasa baada ya Munich Disaster wachezaji karibia wote walipokufa ile sympathy iliwaongezea following so nothing new hapo mkuu alichofanya ni most successfully na longest serving manager of Man U.
Wenger ameshindwa kumaintain nini?? Ofcourse Wenger asingeweza kuwanunua kina Veron; au Kina Rooney ambao kila mtu alikuwa anajua uwezo wao hence pesa yao kuwa kubwa..., Mkuu hapa tunaangalia achievements kulinganisha na resources used.., Sir Alex kapewa muda wa kutosha kwenye timu as well as Funds za kutosha kutumia anavyopenda na kupewa uwezo wa kusema na kufanya anachotaka (na sababu kuna group kubwa la kina Giggs lililoanzia tokea academy) imekuwa rahisi kumsikiliza sababu ni kama baba yao tofauti na siku hizi crop of players ambao hawasikilizi..., Therefore maybe technic ya kumage ya Kina Special One na Wenger ya kuwa rafiki na wachezaji na kuwasikilizia works easier kuliko udikteta wa Sir Alex.., currently ni vigumu kufanya kazi
tukianza kuimagine..., basi ngoja tuimagineKitu alichokifanya Ferguson kuchukua kombe scotland ni kama vile Benitez alivyochukua kombe Spain na
valencia, au hapa Bongo timu zaidi ya Watani wa Jadi ichukue kombe, you must give Credit to that.
Imagine Flamini na Hleb wasingehama Arsenal, imagine nyuma yao acheze Fabregas , kukamilisha diamond awepo RVP, Arsenal ingetisha sana zaidi. Hakuna siginificant age layers Arsenal zinazoleta matumaini ya sasa na future.