wadau mara nyingi nimeona watu wakiadhimisha arobaini ya mtu aliyefariki, je hii ni tamaduni au ni mafundisho ya dini? je jamii nyingine duniania wana utaratibu huu.
sina uelewa mkubwa sana... lakini siku arobaini limekaaa sana kidini na ss hv inaenda pia kuwa kama utamaduni .... ingawa hasa kwa waislam kwani wakristo hawana kitu kinachoitwa arobaini lakini kwa waislam arobaini ni kwa kuzaliwa au kufa kwa binadam lazima iadhimishwe.................... ila ss hv wote christian na islam wanafanya hivyo ingawa sio wote
i have just asked 'mwanazuoni' (muislamu) kuhusu hiyo kitu,ameniambia haipo katika vitabu vyao (mimi si muislamu) ila ni mazoea tu lakini si dhambi ila ni very unpleasant kama mtu ataingia kwenye madeni kuadhimisha hiyo kitu. yes, **** baadhi ya wakristo tunafanya hivyo lakini pia si taratibu ya kidini. Therefore nafikiri ni utamaduni wa mtazania tu........nice try,eeh???
ni tamaduni, wengine huwa wanakuwa wanaiweka familia ya deceased sawasawa, wengine wanagawa mali, wengine wanakula chakula kilichowekwa kautumbo ka maiti yule kwenye wali etc, kila mtu ana desturi yake...
Tuwe tunajadili mambo humu jamvini kwa kuzingatia taratibu zilizopo humu na si kujifurahisha. Mtu aliyefariki siku 40 zilizopita utumbo wake uliwe leo hii na binadamu mwenye akili timamamu inaingia akilini kweli? Tafadhali naomba unieleweshe hapo ubungoubungo.