Usidanganyike TAKUKURU ni mafisadi namba mmoja. Watakukamata kama hujawapa rushwa. Nashukuru Mungu niliwahi kuwa nao japo kwa mda mfupi...kuna siku tulikuwa training pale Morogoro chuo cha TANESCO, Hosea alikuwa akitoa lecture alisema kitu mpaka nikatishika na kukosa interest nao na hatimaye nilijiondokea. Anasema, "hapa ndo mnaanza kazi, miaka miwili tu unakuta mtu gari mpya! Unajiuliza huyu kijana na kamshahara haka hili gari kapata wapi!". Wakati huo yy alikuwa mkurugenzi wa upelelezi, nikajua kwa kuwa alijua hilo tatizo, basi watatafuta jinsi ya kuliondoa...wapi bwana. Niliokuwa nao wakati huo.....baadhi ni matajiri wa kutisha! Hivi ulishawahi kusikia wamekamatana kwa rushwa?
SINA IMANI NA TAKUKURU. Period!