Ardhi na Chakula ndio chanzo cha VITA duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ardhi na Chakula ndio chanzo cha VITA duniani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gogomoka, Jul 11, 2011.

 1. g

  gogomoka Senior Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Taifa lafungwa kitanzi

  Na Restuta James
  11th July 2011B-pepeChapa Maoni Ni mkataba wa kutoa ardhi ya ubwete

  Yatolewa kwa wawekezaji wa kigeni
  Hekta moja kulipiwa kodi Sh. 700 tu

  Wakati Taifa likibeba mzigo wa mikataba mibovu na kusaka njia ya kutoka kwenye kitanzi hicho, tatizo hilo linaonekana kuwa kama donda ndugu baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, mkoani Rukwa kujipiga kitanzi cha mkataba wa kimataifa

  kwa kukodisha sehemu kubwa ya ardhi yake kwa miaka 99, chini ya sheria za kimataifa.

  Uchunguzi wa NIPASHE umebaini kwamba tayari makubaliano kati ya mkodishaji wa ardhi hiyo ambaye ni kampuni ya Agrisol Energy LLC ya Marekani na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwenye maeneo ya Katumba hekta 80,317 na Mishamo hekta 219,800 ambayo yalikuwa makambi ya wakimbizi yamekwishafikiwa.

  Kati ya masharti ya msingi ‘magumu' ambayo yanakiweka kipande hicho cha ardhi rehani ni utata wa kisheria ambao unaeleza kuwa ikiwa mgogoro utatokea kati ya mwekezaji na Halmashauri, itatumika busara na kama itashindikana shauri hilo litaamuliwa na msuluhishi, jijini London, Uingereza.

  "Kutumia busara kutatua mgogoro, ikishindikana itapelekwa kwa msuluhishi ambaye atakuwa Chemba ya Biashara ya Kimataifa (International Chamber of Commerce), usuluhishi utafanyikia London Uingereza," inaeleza sehemu ya makubaliano kati ya Halmashauri na kampuni ya Agrisol, yaliyofikiwa Julai, mwaka jana.

  Mbali ya utata huo wa kisheria, mwekezaji huyo ambaye amejieleza kwamba anamtaji wa dola za Marekani milioni 700, analazimika kulipa Sh. 200 kwenye Serikali Kuu kama kodi ya ardhi kwa ekari na Sh. 500 zitalipwa kwa Halmashauri kwa ekari. Jumla Sh. 700 kwa ekari.

  Hata hivyo, mkataba huo hauelezi kiasi hicho cha fedha kitalipwa kwa muda gani yaani kwa mwezi au kwa mwaka.

  Sharti lingine analopewa mwekezaji ni kutoa msaada wa kijamii kwa wananchi wanaozunguka eneo la uwekezaji.

  "Halmashauri inaitaka Agrisol kila mwaka kuweka mpango wa kujenga uwezo wa wakulima na maafisa ugani pamoja na kuzisaidia taasisi za serikali na kutoa soko kwa mazao ya wakulima," inaeleza taarifa ya Halmashauri ya Mpanda.

  Taarifa ya makubaliano hayo inaeleza kwamba utafiti wa kina dhidi ya kampuni ya Agrisol pamoja na ziara ya nchini Marekani iliyofanywa na baadhi ya madiwani na watendaji wakuu wa Mpanda, mwaka jana umebaini kwamba kampuni hiyo ni makini na ina nia ya dhati ya kuwekeza nchini.

  "Baada ya majadiliano ya kina na kuona umuhimu wa uwekezaji wa kilimo kikubwa wa aina hii na umakini wa wawekezaji wanaotarajiwa, imekubalika mkataba wa makubaliano wa awali usainiwe wiki mbili kuanzia Julai 20, 2010 ili kuepuka mwekezaji kukosa fedha alizoomba kwenye taasisi za fedha kiasi cha dola za Marekani milioni 700."

  Inaeleza zaidi kwamba "imekubalika kwamba upembuzi yakinifu uanze mara tu baada ya kusaini makubaliano ya awali."  MAONI YA JUMLA

  Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ambao walikuwa kwenye ziara nchini Marekani, ‘wanaipigia debe' kampuni hiyo kwamba mwekezaji huyo ni makini.

  "Wana dhamira ya kweli ya kuwekeza nchini kwani wangeweza kwenda na kuwekeza katika nchi nyingine walizokubaliwa kama Brazil, Argentina na Msumbiji," inaeleza taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo inafafanua kwamba mwekezaji atalazimika kulima mazao ya chakula na kuendesha shughuli za kilimo zaidi.

  Watendaji wa Halmashauri ya Mpanda ambao walipelekwa Marekani na kampuni ya Agrisol ni Katibu Tawala mkoa wa Rukwa, Salum Chima, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Dk. Rajab Rutengwe, Mwenyekiti wa Halmashauri, Philip Kalyalya, Emmanuel Kalobelo na Mwanasheria wa Halmashauri, Patrick Mwakyusa.

  Wengine ni Ofisa Mipango wa Halmashauri, Huruma Mwalutanile, Ofisa Kilimo na Mifugo, Fabian Kashindye, Mwenyekiti Kamati ya Maadili, Teddy Nyambo, Mjumbe wa Kamati ya Fedha, Rose Mayaya na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Sylivester Nswima.

  Hata hivyo, pamoja na viongozi hao kueleza nia ya uwekezaji huo ni mazao ya kilimo, utafiti zaidi unaonyesha kuwa kampuni ya Agrisol Energy LLC, inajishughulisha na masuala ya nishati ikiwemo kilimo cha jatrofa kwa ajili ya kuzalisha mafuta ya ethanol.

  Mbunge wa Mpanda Mjini (Chadema), Said Arfi, ambaye mara kadhaa amekuwa akipigia kelele uwekezaji huo, alipoulizwa kuhusiana na hatua ambayo imefikiwa hivi sasa, alisema inashangaza na kusikitisha kwa kuwa uwekezaji huo unawaacha wananchi kuwa manamba na watumwa ndani ya nchi yao.

  "Ardhi inagusa maslahi ya wananchi wengi, tuna migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, ardhi hii ingeweza kupewa wakulima…nadhani hili lingeangaliwa ili tusirudie makosa ya nyuma kwa kumilikisha ardhi kubwa kwa wachache wakati watu wengi wakiteseka," alisema.

  Alisema "Kwa uwekezaji huu, hivi serikali itawezaje kuwazuia vijana wasije mjini? Mimi nimekuwa nikishauri kila wakati kwamba ingekuwa bora zaidi kama ardhi ile ingegawiwa kwa vijana, halafu wakapewa zana na mbegu bora hakuna atakayekuja mjini."

  Arfi alisema inashangaza kuiona serikali ikipigia debe kilimo kikubwa kwa kutafsiri dhana ya kilimo kwanza, ambacho hakiwanufaishi wakulima wengi wa kizalendo.

  Arfi alisema ukodishaji huo ni sawa na uporaji wa ardhi kwa kuwa Watanzania pia wanao uwezo wa kulipa Sh. 700 ambazo mwekezaji anaelezwa kulipa.

  "Hivi ni kweli Watanzania wakimilikishwa maeneo haya watashindwa kulipa Sh. 700? Rasimu ya mkataba inaonyesha mgogoro ukasuluhishwe London wakati ardhi iko Mpanda Tanzania, hii kasumba itaisha lini hata vyombo vyetu vya haki hatuviamini?" alihoji.

  Alisema mkataba huo hauelezi mali zilizopo kwenye maeneo hayo, zikiwemo shule, stesheni ya reli, zahanati na maghala "yamenunuliwa na mwekezaji au amepewa kama zawadi?

  Hata hivyo, alisema ni vyema Tanzania ikajifunza kutoka Zimbabwe kwa kuzingatia ongezeko la watu na ardhi iliyopo.


  Wakuu; hivi viongozi wetu wanatupeleka wapi???? Kwa mwendo sitashangaa kwa kipindi cha miaka michache ijayo Watanzania tutachinjana wenyewe kwa wenyewe. Hivi umeshawahi kusikia Rukwa kuna njaa ndani ya Tanzania? Rukwa ndio food bowl ya Tanzania. Leo hii tunauza ardhi fertile. Naomba Watanzania wenzangu na hasa wana CCM wanakubaliana na hili janga la njaa tunalojitakia?????

  Nawasilisha.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  migogoro na vita duniani vinasababishwa kwa kiwango kikubwa na rangi ya ngozi, ardhi na chakula vina-trail, angalia usikosee kuelewa.
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  the best creem of black people wiped out by slavery, ndo maana mkienda bagamoyo mnachekacheka tu, hakuna aelimikae
   
Loading...