APR vs Yanga mara ya pili Ligi ya Mabingwa, pambano la 8 la daima!

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Yanga-wakisakama-goli-la-Apr.jpg

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga, watapambana na mabingwa wa Rwanda, Armée Patriotique Rwandaise (APR), katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufuzu raundi ya awali kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius.

APR yenyewe imefuzu hatua ya awali kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-2 dhidi ya mabingwa wa Swaziland, Mbabane Swallows. Mechi ya kwanza walifungwa ugenini bao 1-0, lakini Jumamosi, Februari 27, 2016 wakaichabanga timu hiyo mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali.

Mechi ya kwanza baina ya APR na Yanga itachezwa mbele ya mashabiki 30,000 kwenye Uwanja wa Amohoro Machi 12, 2016 na inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na rekodi nzuri ya APR ya kufanya vizuri nyumbani.

Kwamba hiyo inaweza kuwa tiketi ya Yanga kubaki ama kuondoka mashindanoni ni suala la kusubiri kutokana na rekodi baina ya timu hizo mbili zenye uzoefu tofauti wa mashindano ya ndani na kimataifa.

Hii itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kupambana katika mashindano ya Afrika, hususan Ligi ya Mabingwa, lakini itakuwa mechi ya nane kuzikutanisha timu hizo katika mashindano yote.

Katika mechi saba zilizopita...INGIA NDANI
 
Cha ajabu Yanga kupokelewa na mashabiki lukuki na mechi kuoneshwa 'live' huko ni sahihi. Ila tusubiri mechi ya pili kama 'live' itakuwepo na APR kupokelewa kwa mbwembwe!
 
APR wanachezea kichapo kama walichokipata Simba hapo hapo kwao Amahoro, wakija Dar tunapiga tena mbili halafu mchezo unaishia hapo.
 
Back
Top Bottom