Apps muhimu sana kama simu yako ina root access

Apps muhimu sana kama simu yako ina root access

Strictly Syrup

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
1,227
Reaction score
1,821
Je umekwisharoot Android device yako (Smartphone/Tablet)

2j4tzk7.jpg


Topic za Android Rooting imekuwa zikijadiliwa sana hapa jukwaani. Lakini mtu anaweza akawa amesharoot simu yake lakini asifahamu kwamba kuna apps muhimu sana za kuttumia kwenye simu yako kama una root access. Nitaziainisha baadhi ya apps nilizoziona muhimu sana.

1. AdAway
s5zq07.jpg


Advertisements nyingi utazikuta kwenye apps zinazotolewa kama free version. Kwa hiyo developers wataweka support y aAds kukuinfluence wewe kununua apps zao. Kwa hiyo, App hii itakusaidia kuondoa matangazo yote yanayokuwa yanakusumbua pindi utumiapo Apps au ukicheza games mbalimbali.

2. Uninstall Master
wwnmv9.jpg


Ukiwa na Application hii, Utaweza kuondoa bloatwares zote pamoja na system apps usizozitaka/usizozitumia. Ni vizuri kuwa mwangalifu kwa kuwa unaweza ukabrick device yako endapo utafuta system files muhimu.

3. Greenify
2wedtsl.jpg


App hii ni muhimu sana katika kupunguza matumizi ya battery yasiyo ya muhimu. App hii inaziweka sleep mode apps zote zinazokuwa zinarun background na kutumia kiasi kikubwa cha power katika simu yako.

4. ROM Manager
j9sol5.jpg


Kama umesharoot simu yako na unataka kuingia kwenye ulimwengu wa Custom ROMs, ninakushauri utumie app hii. App hii inapatikana kwa free na Premium versions. App hii itaweza kukusaidia Kubackup stock ROM yako, incase kama utapenda kuja kuitumia tena. Itakusaidia kukutafutia custom recovery kwa ajili ya simu yako na kuiflash. Itakusaidia kufanya partition ya SD Card yako. Pia kikubwa kabisa nilichopenda katika hii app ni kwamba, kama unatumia premium version, app hii itakupatia Custom ROMS zote ziapatikanazo kwa simu yako.

5. Avast Anti-Theft
x4qb07.jpg


Kwa wale mliochoka na wezi wa simu app hii itakusaidia; kutrack na kulocate simu yako iliyopotea,kulock au kuwipe vitu vyote kwenye simu yako mengine mengi kama kurecord au kuchukua picha za eneo simu yako ilipo kupitia simu yako. App hii itakutaarifu haraka kwa email endapo line yako itaondolewa kwenye simu yako (kubadilishwa)

6. Recovery Tools
App hii inafanana kidogo na ROM Manager kwa feature moja, ni kwamba app hii ipo advanced zaidi katika kuweka recoveries. App hii itasearch recovery images online kisha itaorodhesha recovery zote zinazopatikana kwa simu yako. Kama utapenda TWRP, Clockworkmod, Phils na hata ukitaka kuweka Stock Recovery yako tena. Na hata kama utapenda kuweka recovery iliyopo kwenye storage yako, eg. SD Card utaumia app hii kulocate na kuflash recovery images yako.

Apps nyingine muhimu ni kama Lucky Patcher. Ambayo inafanya patches kwenye apps mbalimbali kuzuia license verification. App hii imejulikana sana baada ya kuweza kupatch premium app maarufu sana ya music iitwayo Poweramp.

s5ffac.jpg


2hqtmwk.jpg
 
Mkuu Dream Chaser ,hii ya ROM MANAGER PREMIUM inawezesheza kuinstall custom rom au inafanya vipi ,maelezo yamenipenya hapo!
 
Titanium Backup Pro inasaidia kubackup apps zako endapo zikifutika unazipata tena
 
Titanium Backup Pro inasaidia kubackup apps zako endapo zikifutika unazipata tena

kama una cwm recovery basi nandroid manager ni chaguo mahususi kwa ajili ya backup ya data, system na apps bila kusahau settings
 
kama una cwm recovery basi nandroid manager ni chaguo mahususi kwa ajili ya backup ya data, system na apps bila kusahau settings

Nlikuwa nazo nikashindwa kuzitumia… nimefanya wipe data… nkabak mtupu
 
Mimi naomba maelekezo zaidi namna unavyoweza kuondoa hayo matangazo yanayojitokeza kwa kweli ni kero sana

Nenda google search kitu inaitwa adaway apk then install kwa simu yako hayo matangazo utayajisikia kwa jirani but hakikisha simu yako ipo rooted
 
kama una cwm recovery basi nandroid manager ni chaguo mahususi kwa ajili ya backup ya data, system na apps bila kusahau settings

Mtaalam C 6 naomba utupie namba yako hapa 0754604475
 
Warrior ina maana hizi app zote hadi simu yako iwe rooted au iwe inauwezo wa kufanya rooting?

Je mwizi akiwahi mapema akafanya Factory reset hiyo Avast Anti-Theft , je itafanya kazi tena?
 
Ivi app ya tigo pesa. Ukiidownload kutoka play store inaweza kukuwezesha kukopa hela. Au unakopa kwa namna ipi. Msaada.
 
Ivi app ya tigo pesa. Ukiidownload kutoka play store inaweza kukuwezesha kukopa hela. Au unakopa kwa namna ipi. Msaada.
kukopa sio lazima uwe na app wewe piga *150*81# kisha fuata maelekezo kama unasifa watakupa mkopo
*vigezo na masharti kuzingatiwa
 
Back
Top Bottom