ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
APPLE WACHOMOA UBORESHAJI WA IOS 8.01
Wiki moja baada ya kutoa iOS 8 Apple wamelazimika kuboresha (update) OS hiyo na kutoa iOS8.01, lengo la uboreshwaji huo lilikuwa ni kuondoa baadhi ya matatizo yaliyojitokeza kwenye iOS 8, ikiwa ni pamoja na simu na iPad mbali mbali kupoteza mtandao wa WiFi na pia betri kumalizika haraka. Matatizo haya yamejitokeza kwenye baadhi tu ya gajeti za zamani za Apple na si kwenye iPhone 6 au iPhone 6 Plus.
Mara baada ya kuboresha iOS 8 kwenda 8.0.1 watumiaji mbali mbali waligundua matatizo mawili makubwa, kwanza simu hazikuweza kuunganisha huduma za simu yaani zimekuwa hazina mtandao na pia Touch ID imeacha kufanya kazi. Hivyo mara baada ya kupakia toleo hilo la iOS iPhone hugeuka kuwa iPod Touch. Muda mchache baadae mzungumzaji wa Apple alikiri tatizo bila na kueleza kwamba wanafanya uchunguzi juu ya taarifa hizo na wameiondoa iOS 8.0.1 kutoka kwenye server zao.
Apple mpaka sasa hawajatoa kauli yoyote kuhusu Bendgate, mashirika makubwa ya habari ulimwenguni kwama vile BBC na CNN tayari yamesharipoti tatizo hili wengine wakianza kutabiri huenda Apple watatoa makava ya bure kwa wanunuaji wa iPhone 6 Plus.
Hii si mara ya kwanza kwa Apple kutoa boresha kisha kuliondoa. Miaka kadhaa iliyopita Apple walilazimika kuiondoa app ya Maps na kuomba radhi baada ya App hiyo kuwa na matatizo mengi mno. Kashfa hii ilipelekea vigogo kadhaa kufukuzwa kazi Apple. Tunaamini si muda mrefu kuanzia sasa iOS 8.0.1 itarudishwa tena baada ya kufanyiwa marekebisho. Iwapo una gajeti ya Apple yenye kutumia iOS basi ushauri wetu ni kuwa itakapotoka tena subiri siku kadhaa zipite kabla ya kuboresha iPhone, iPad au iPod touch yako.
Chanzo:gajetek habari
