Apple kuzindua iphone 13 leo

Apple kuzindua iphone 13 leo

Cash Generating Unit

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
13,285
Reaction score
39,491
Kampuni ya apple leo itakua na uzinduzi wa bidhaa zake mpya zitakazoingia sokoni. Bidhaa hzo ni kama iphone 13, iphone 13 min, iphone 13 pro na iphone 13 pro max.

Apple wamesema iphone 13 haitakua na mwonekano mpya hvo toleo hili wamejikita katika kuboresha camera kuwa na uwezo mkubwa, procesa yenye spidi na betri ambayo itakaa kwa muda mrefu.

Bidhaa zingine zitakazo tambulishwa ni apple watch, macbook, airpod na ipad

Kikubwa zaidi ni ujio wa ios 15 kwenye iphone 13, tukio litaanza saa2 usiku kwa Africa mashariki. Kazi kwenu.
 
Kama zile leaks za iPhone 14 ni za kweli... soko la hizi iPhone 13 litadolola sana.

Si kwa design ile... 14 ni kali sana
 
🙄🙄🙄Yani washafika iPhone 13 nasijawah miliki ata iPhone 1🥴🥴life is not fair 😔😔😔
😂😂😂jiongeze chapu huoni mwenzio anachangamkia fursa hapo juu.

By the way Usiuze utu kwa vitu kama simu havina tofauti na musiki utacheza wee kesho mond anaachia goma jingine.
 
Kama zile leaks za iPhone 14 ni za kweli... soko la hizi iPhone 13 litadolola sana.

Si kwa design ile... 14 ni kali sana
achana na video za concept mkuu,ni ndoto tu za watu zile kwenye video,hazina uhalisia wowote.
 
Achana na video za concept mkuu,ni ndoto tu za watu zile kwenye video,hazina uhalisia wowote.

Kweli maana ni mapema mno. Mzigo wa mwakani unavuja wakati hata wa mwaka huu bado haujatoka .
 
Mbona hawa jamaaa creativity hakuna tangu afariki Mzee Jobs mpaka leo Notch haiondoki inapunguzwa tu, kazi yao kuleta new bionic chips, iPhone 11 to 12 hawakuongeza betri sasa hivi wameongeza battery kidogo mambo ya kusema wanaongeza brightness by 28% yashatuchosha.

Ndio maana Samsung wana wamock wanasema wanaona De javu maana mambo yaleyale eti
 
Back
Top Bottom