ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Apple inayumba Ingawa Bado ni Kigogo
Apple wametangaza mambo mawili makubwa, awali wametangaza matokeo ya mapato katika robo ya kwanza ya mwaka 2013. Pili wametangaza mkutano rasmi wa watengenezaji wa programu za iOS na Mac OSX unaojulikana kama World Wide Developers Conference (WWDC). Kwa kawaida Apple inapotoa matangazo kama haya huwa ni wakati ambao kampuni hiyo huonyesha uwezo wake mkubwa kama moja kati ya kampuni kigogo katika teknolojia Duniani, lakini safari hii kuna hali ya mchanganyiko, yapo yenye kuonyesha umwamba wa Apple na pia yapo mambo ambayo ni ya kuvunja moyo.
Tim Cook katika tangazo la mkutano wa WWDC ambao utaanza tarehe 10 mwezi Juni na kumalizika tarehe 14 mwezi huo huo, akiripotiwa na Engadget Distro, ameweka wazi kuwa wadau wasitarajie bidhaa yoyote mpya na badala yake Apple watatoa bidhaa mpya katika kipindi cha mwezi wa tisa. Wengi miongoni mwa wanateknolojia walitarajia kuwa Apple wangetoa iWatch, iPhone mpya, iPad Mini 2 au iPad 5, hivyo tangazo hili sio tu limevunja moyo bali pia limezima kila aina ya tetesi na uvumi unaohusiana na bidhaa mpya zinazotarajiwa kutolewa na Apple mwezi Juni.
Pia tangazo hili maana yake Apple wameipa Samsung Galaxy S4 nafasi kubwa ya kutamba katika mauzo kwa karibu miezi mitano mpaka sita. Iwapo Apple watatoa iPhone 5S basi itakuwa ni vigumu kuyafikia mauzo ya Galaxy S4 ingawa uwezekano wa kuyafikia mauzo kwa iPhone 6 ni mkubwa. Tofauti ya 5S na 6 ni kwamba 6 itafanyiwa mabadiliko makubwa wakati 5S ni simu ile ile yaani iPhone 5 lakini itaongezwa kasi tu. Hatuelewi ni kwa nini Apple huipa nafasi kama hii Samsung wakati katika tableti Apple walifanya mkakati mzuri wa kuzuia mauzo ya Microsoft Surface kwa kutoa iPad With Retina Display muda mchache kabla ya kutoka kwa tableti hiyo, iPad hii ilitolewa kinyume na ratiba ya kawaida ya Apple hivyo ni wazi ililenga kwenye upinzani wa kibiashara badala ya mauzo ya kawaida. Pia Apple walitoa iPad Mini kuhimili mauzo ya utitiri wa tableti ndogo za Android kama vile Nexus 7, Amazon Kindle Fire na Samsung Galaxy Tab 2 - 7.0.
Kwa mujibu wa jarida la Engadget Distro; akijibu maswali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Apple Tim Cook pia ameeleza wateja wasitarajie iPhone kubwa zaidi mwaka huu kwa vile unapoongeza ukubwa wa simu basi hupelekea kupoteza ubora wa skrini na apps pia haziwezi kufanya kazi na skrini hiyo mpaka pale watengenezaji watakapozifanyia marekebisho. Katika suala la ubora wa skrini hatuelewi ni kwa nini Cook ametoa madai kama haya, hii ni kutokana na ukweli kwamba tayari kuna simu kama vile Sony Xperia Z ambayo ina skrini kubwa na bora kuliko ile ya iPhone 5.
Lakini Cook yuko sahihi katika suala la apps kutofanya kazi kwa usahihi katika ukubwa mpya wa skrini, kwani mpaka sasa kuna maelfu ya apps ambazo bado huonyesha weusi juu na chini ya sehemu ya skrini katika iPhone 5 kwa vile watengenezaji wake hawakufanya marekebisho au uboreshwaji waliotakiwa kuufanya. Hii ina maana kwamba apps ambazo zinafanya kazi kwa ufanisi na iPhone 5 ni chache ukilinganisha na zile zinazofanya kazi na iPhone zenye skrini ya inchi 3.5 yaani iPhone 4S kurudi nyuma.
Hata hivyo kwa upande wa iPad Mini hali haikuwa hivyo kwani iPad hiyo imepewa rizolushani sawa na zile za iPad 2, hivyo watengeneza apps hawakuhitaji kufanya chochote ili apps zao zifanye kazi kwa usahihi katika iPad Mini. Hivyo hii maana yake ni kwamba ingawa iPad Mini ni ndogo kuliko iPad 2 lakini Mini ina skrini bora kuliko iPad 2. Hili kulitekeleza kwa upande wa iPhone ni gumu, kwani ukiongeza ukubwa na kuacha rizolushani zile zile ndio ubora wa skrini hupotea na si rahisi kuipa skrini ya ukubwa wa inchi 5 kwa mfano rizolushani sawa na za iPad kama ilivyofanyika kwenye iPad Mini. Hii pia maana yake ni kwamba iPad Mini kuwa na kioo cha retina itakuwa ni jambo gumu kidogo, ingawa linawezekana
Kwa upande wa ripoti za fedha Apple imetangaza faida ya Dola bilioni tisa na nusu, sambamba na hili Apple pia imeuza iPhone milioni thelathini na saba na laki nne (milioni 37.4) na iPad karibu milioni ishirini. Wakati mauzo ya iPad na iPhone ni yenye kuridhisha na kuonyesha Apple bado ni kigogo, faida kubwa iliyopatikana bado ni pigo kwa Apple kwani ikilinganishwa na kipindi kama hichi mwaka jana faida ya kampuni hiyo imeteremka. Hata hivyo faida ya bilioni tisa maana yake Apple si kampuni ambayo inaweza kuelezewa kwamba inaanguka bali ni kampuni ambayo inashindwa kuyafikia mafanikio yake ya miaka iliyopita.
Chanzo: gajetek habari

TSH