Apple hawajamaliza kutoa Bidhaa Mpya 2013

Apple hawajamaliza kutoa Bidhaa Mpya 2013

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159

​
Wengi walidhani tukio maaluma (Special Event) la mwezi uliopita ndio ungekuwa mkutano wa mwisho wa Apple kutangaza bidhaa zao mpya mwaka huu. Huenda Apple bado hawajamaliza kazi kwa mwaka huu, kwa mujibu wa minon’gono iliyosambaa mtandaoni kampuni hiyo inatarajiwa kuitisha mkutano mwengine wa kutangaza bidhaa zao mpya mwezi huu tarehe 22. Iwapo taarifa hizi ni sahihi, hili litakuwa ni tukio la tatu kwa mwaka huu ambapo Apple kwenye matukio ya nyuma walitangaza bidhaa mbali mbali huku wengi wakiwa wamevunjika moyo kwani kinyume na matarajio yao Apple haikutoa iWatch.


Kitakachotangazwa kwenye mkutano huo na timu ya afisa mtendaji mkuu wa kampuni hiy Tim Cook bado ni siri ya Apple, lakini moja la uhakika zaidi ni Mac OS X mpya inayojulikana kama Maverick, OS ambayo inamaliza mtindo wa kampuni hiyo ya kutumia majina ya jamii ya chui, majina kama vile Snow Leopard na Mountain Lion. Mac OS X Maverick inasubiriwa kwa hamu na wengi ambao tayari wanamiliki kompyuta za Apple, Apple kinyume na Microsoft huuza uboreshwaji (upgrade) wa OS kwa bei nafuu mno, toleo la mwisho ambalo ni Mountain Lion liliuzwa £20 (kiasi TSh 50,000) tu nchini UK.



​
Hata hivyo tukio hilo halitakuwa kubwa na Apple inatarajiwa kuwakaribisha waalikwa rasmi tu na sio kila mtu, hakutarajiwi kuwepo na tiketi kama inavyokuwa kwenye mkutano wa watengeneza apps wa WWDC. Apple inatarajiwa kualika wanahabari, washirika (partners) wao pamoja na watu maarufu na wenye michango mbali mbali katika mafanikio ya kampuni hiyo.


Kwa mujibu wa minon’gono na tetesi bidhaa zitakazotangazwa ni pamoja na iPad 5 na iPad Mini 2, wakati iPad 5 inatarajiwa kuwa na umbile la iPad Mini tofauti ikiwa ni ukubwa, iPad Mini inatarajiwa kuna wa Retina Display kama iPad with Retina Display. Wengi wanamatumaini pia bidhaa hizo zitawekewa finger print scanner, ingawa hakuna uhakika wa jambo hili.


​
Bidhaa nyingine ambayo inatarajiwa kutangazwa tarehe yake mauzo si ngeni kwa vile ilishaonyeshwa katika WWDC 2013, bidhaa hiyo ni Mac Pro, kompyuta ambayo ina umbile la kipekee pamoja, nguvu na kasi kubwa. Vile vile pamoja na iWatch kuvuma mno hakuna taarifa zozote kama bidhaa hiyo itatolewa na Apple mwaka huu. Ikiwa taarifa hizi ni sahihi zimebakia siku kadhaa kabla ya tukio hilo.

Chanzo: gajetek habari
​

​
 
tuwasubiri. napenda bidhaa zao hawa jamaa ingawa ni ghali sana.
 
Back
Top Bottom