beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Karani wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), Bakari Mlanga, 23, amehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa kosa la kughushi fomu za Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya (NHIF).
Pamoja na Bakari, mtuhumiwa mwingine ambaye pia ni mkazi wa Manzese, Dar es Salaam, Ahmed Mbinjika, 25, amejikuta akitupwa jela miaka 12 baada ya kupatikana na hatia ya makosa hayohayo.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan ameema mahakama hiyo imefikia kutoa adhabu hiyo baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha tuhuma za watuhumiw hao bila kuach chembe ya wasiwasi kupitia mashahidi watano.
Bakari alikuwa akikabiliwa na mashtaka tisa huku Ahmed alikuwa akikabiliwa na mashtaka manne ambapo kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kila shtaka lililokuwa linawakabili ambapo wamekutwa na hatia katika mashtaka yote.
Awali, Wakili wa Serikali, Florida Wenseslaus alidai kuwa washtakiwa hao walighushi fomu ya NHIF ya Tito Mfilinge ikionesha kuwa imesainiwa na Dkt. Emmanuel Chambenga na kwamba ni halali kutumika huku wakijua ya kuwa sio kweli.