Apata upofu baada ya kumeza dawa aina ya Fansidar

dumila

Member
Jun 10, 2016
15
2
MKAZI WA MLANDIZI KIBAHA PWANI APATA UPOFU BAADA YA KUMEZA DAWA AINA YA FANSIDER AOMBA MSAADA ML.18

MKAZI mmoja ajulikanaye kwa jina la Seleman Mgoto (42) anayeishi katika kitongoji cha Janga
kilichopo eneo la Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ameathirika macho yake mawili na
kupoteza kabisa uwezo wa kuona baada ya kutumia dawa ya kutibu malaria aina ya Fansider
hivyo anahitaji msaada wa kiasi cha shilingi milioni 18 kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu
zaidi nchini India.

Hayo yamebainika baada ya mwandishi habari hizi kuweza kufika nyumbani kwa kaka yake maeneo ya mlandizi ambapo ndipo anapoishi kwa sasa baada ya kupatwa na tatizo hilo na kuweza kuzungumza naye kuhusiana na mkasa wa tukio hilo lililompata.

Akizunguza kwa masikitiko makubwa Mgoto alisema kwamba Mnamo ya Agosti 2012 alikuwa anaumwa na alipokwenda kupimwa aligundulika kuwa na wadudu tisa wa ugonjwa wa malaria ndipo alipoandika dawa aina ya fansider na kuamua kwenda kuzinunua katika moja la duka la madawa lililopo maeneo hayo ya mlandizi na baada ya kuzimeza hali yake baada ya siku mbili ilianza kubadilika kutokana na sumu kali iliyokuwepo mwilini mwake . “Mimi mwezi agosti mwaka 2012 ndugu zangu waandishi niliweza kuumwa na nilipoenda kupima afya niligundulika nina malaria, na baada ya hapo
niliweza kuandikiwa dawa na nikaenda kununua dawa aina ya fansider, ila baada ya siku mbii hali yangu iiweza kubadilika na nilipokwenda kituo cha afya niilazwa kwa ajili matibab zaidi” alisema.

Aidha akifafanua kuhusina na kuangaika katika hospitali mbali mbali kwa ajili ya matibabu alisema kwamba mara ya mwisho alikwenda kuwaona madaktari bingwa wa hospitari ya CCBRT ya jijini Dar es salaam ambapo walimwambia macho yake kwa hapa Tanzania hayawezi kutibiwa mpaka aende nchini India ndio yanaweza kupona.

Pia katika hatua nyingine amesema kwamba kwa sasa maisha yake yamekuwa ni magumu sana kutokana na kutokuwa na kipato chochote kile anachokiingiza ukizingatia ana familia mke pamoja na watoto watatu ambao wanamtegemea kwa kila kitu ambapo watoto wengine wawili wapo wanasoma sekondari hivyo kunahitajika mahitaji mengine ya msingi.

Mwenyekiti wa kamati maalumu ya kumsaidia kwenda kupatiwa matibabu nchini India Eria Chaofu pamoja na Luiza Mdachi ambaye ni dada yake wamesema kwamba familia imeangaika kwa hali na mali kwa kipindi cha miaka mitatu katika hospitali mbali mbali kwa ajili ya kumtibia bila ya kupata mafanikio yoyote kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha. miaka mitatu.

Aidha Mwenyekiti huyo amemwomba Rais wa awamu ya tano Dr.John Mgufuli kumsaidia mgonjwa huyo pamoja na wadau wengine wakiwemo wakuu wa wilaya, wabunge, wakuu wa miko pamoja na Wizara ya afya ili aweze kwenda kutibiwa na kurudi katika hali.

Kwa mtu yoyote ambaye ameguswa na anahitaji kumsaidia mchango wake kwa hali na mali Seleman Mgoto ambaye amepoteza uwezo wa kuona kabisa wa macho yake mawili,atume kwa tigo pesa -0655-413939 au M-PESA 0754-413939 na akaunti namba NMB -80110000915 kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu nchini India kwani zinahitajika shilingi milioni 18.

Nimerusha katika magroup ya wabunge na magroup mengine.
 
Back
Top Bottom