Naombeni mnijuze juu ya bei ya kupanga apartment za NHC kama zle za shekilango na taratibu za kufuata. Asanteni
Mkuu ofisivza kinondoni zipo sehem gani?Mleta mada na wanaJF wengine,
NHC wana utaratibu wa kuuza na kupangisha nyumba.
Hivyo kwa upande wa kuuza, mara zikiuzwa zinakuwa mali ya mmiliki na ni mmiliki tu ndiye ataamua nini afanye na apartment yake (aidha apangishe ama aishi yeye). Mfano wa hizi apartments ndio kama za pale Shekilango, Mchikichini, Upanga nk
Lakini kwa zile za kupangisha utaratibu uliopo ni kwenda kwenye ofisi ya mkoa ambao ungependa kupanga nyumba ( NHC uwa wanatambua Ilala, Temeke, Kinondoni na Upanga kama mikoa)....ukifika ulizia ofisi za estate....utalipia fomu ya maombi ya upangaji kiasi cha TZS 2500 na utatakiwa kujaza fomu hiyo ya maombi....kisha utasubiri mrejesho kutoka kwa maofisa wa NHC kukuarifu kama umepata upangaji ama lah.
mimi nilishawahi kuomba nikalipa hiyo fee, ebwana hadi leo sijawahi pata mrejesho positive...kila mara nyumba ya kiwango chako hamna..nilitaka ya 200,000. wanasema kwa kiwango hiki na kushuka chini watu waliopo hawahami....pia hizo mpya ngumu kupata..watu wanatoa oda kinyemela tu Usipojuana na watu utaishia kulipa sh 2500 na kubaki ukisubiri tu. Ila nadhani kwa apartments za gharama kidogo zinaweza kuwepo.
We nawe hujui mipango mjini..watu tu a wiki toka tumehamia kwenye new flat hapa shekilango na bado apartment nyingi tu ziko wazi
We nawe hujui mipango mjini..watu tu a wiki toka tumehamia kwenye new flat hapa shekilango na bado apartment nyingi tu ziko wazi