Antibaotiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Antibaotiki

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  Kifua kikuu au TB ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na vimelea viitwavyo Mycobacterium tuberculosis.
  Yaliyomo  Kuna aina mbili za Kifua kikuu(TB)


  1. TB ya mapafu
  2. TB ya nje ya mapafu(hii hutokea sehemu yoyote ya mwili nje ya mapafu)

  • TB ya mapafu imegawanyika sehemu mbili
   • TB inayoambukiza (ambayo vimelea vinagunduliwa) katika makohozi(Kifua kikuu) ambayo ndio TB ya hatari zaidi na ni kiasi cha asilimia 90 ya aina zote za TB.

   • TB isiyoambukiza na vimelea haviwi katika makohozi.
  Chanzo cha Maambukizi ya Kifua kikuu(TB)


  • TB inaambukizwa kwa njia ya hewa kutoka kwa mgonjwa mwenye Kifua kikuu kwenda kwa watu wengine. Hali hii hutokea hasa katika sehemu zenye msongamano wa watu au nymba ambazo hazipitishi hewa na mwanga wa kutosha.
  Dalili ya TB ya Mapafu(Kifua kikuu)

  Dalili ya madhara ya kifua kikuu ni kama zifuatazo:

  1. Kukohoa mfululizo kwa muda wa wiki mbili au zaidi
  2. Kutoa makohozi mazito au yaliyochanganyika na damu
  3. Kutokwa na jasho jingi kuliko kawaida usiku wakati mtu amelala
  4. Maumivu ya kufua
  5. Kukosa hamu ya kula
  kukonda na kupungua uzito wa mwili

  1. Mwili kunyong'onyea na kuhisi uchovu bila ya sababu maalumu
  2. Homa za wakati wa jioni
  3. Kuishiwa na pumzi au kupumua kwa shida
  Tiba

  Kifua kikuu kinatibika na kupona kabisa kwa kupata dawa za zinazopatikana katika hospitali.

  Chanzo: Kifua kikuu - Wikipedia, kamusi elezo huru
   
Loading...