MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Nadhani kuna baadhi ya wafanyakazi kama Anne Malecela bado wanaishi jana lakini wanafanya kazi leo.
Nimeshangaa sana kumsikia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela akidai Mkoa wake hauna hata mfanyakazi hewa mmoja wakati siku nne zilizopita alisikika kwenye vyombo vya habari akidai majina ya wafanyakazi hewa anayo na Wakurugenzi wa Halmashauri wasijisumbue kumdanganya.
Yaani Mkuu wa Mkoa anakaa ofisini akisubiri repoti kutoka kwa Wakurugenzi/Makatibu Tawala ambao ndio watuhumiwa wa kutengeneza wafanyakazi hewa eti wampelekee majina ya wafanyakazi hewa ili wajikaange wenyewe kwa mafuta yao. This is fun to say the least.
Baadhi ya Wakuu wengine wa Mkoa wamehakiki wao wenyewe lakini Mama yetu Anne Malecela bado anafanya kazi za kimazoea za awamu ya nne ambazo zilikuwa zinachagizwa na legerdemain and irresponsible.
Haiwezekani katika Tanzania Bara nzima ambayo mikoa yote ina wafanyakazi hewa halafu Mkoa wa Shinyanga pekee wenye Wilaya tatu na Halmashauri sita usiwe na mfanyakazi hata mmoja ambaye ni hewa. Hii hata kimantiki haiwezekani hata kidogo.
Either amedanganywa na wakurugenzi au ameshirikiana na wakurugenzi kuficha uozo wao.
Hata kama umedanganywa au umeshirikiana na Wakurugenzi kuficha uozo naomba utambue kuwa utabeba mzigo wao. Rais Magufuli hawezi kukuangalia usoni wakati akikutumbua.
Inafaa Rais Magufuli aunde kikosi maalum ambacho ni independent ili kikafanye verification katika kila mikoa kuhakikisha kama repoti waliyoleta Wakuu wa Mikoa ni kweli au usanii. Haiwezekani Wakurugenzi ambao ni watengeneza wafanyakazi hewa eti wawe ndio watafuta wafanyakazi hewa.
Hii hapa chini ni habari kuhusu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango akisema anafahamu majina ya wafanyakazi hewa.
Nilimtahadharisha mapema Mama yetu Anne Malecela lakini akaamua kuweka pamba masikioni.
Rais Magufuli ametengua uteuzi wake baada ya kuwa Mkuu wa Mkoa kwa muda wa wiki tatu (ametumbuliwa)

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela ametoa siku sita kwa Wakurugenzi wa Halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na Kahama zilizopo wilayani Kahama kuhakikisha wanawakilisha kwake majina ya watumishi hewa ifikapo Jumatano ijayo.
Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa halmashuri zote tatu za Wilaya ya Kahama muda mfupi baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja ya kukagua shughuli za maendeleo wilayani Kahama, ikiwa ni sambamba na kuwapa pole waathirika wa mvua kubwa ya mawe katika kijiji na Kata ya Mwakata.
Mvua hiyo ya mwanzoni mwa Machi mwaka jana ilisababisha maafa makubwa, ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 38 na kujeruhi wengine zaidi ya 80.
Kilango alisema lundo la watumishi hewa katika halmashauri hizo halikubaliki, hivyo ni wajibu wa wakurugenzi kuhakikisha kuwa majina yao yanawakilishwa ofisi ya mkuu wa mkoa sambamba na maelezo ya kumbukumbu zao za ajira, wanavyolipwa na kiasi wanacholipwa.
“Hata wakurugenzi wakiwaficha, tayari orodha yao ninayo mezani…naomba mniletee majina,” alisema mkuu huyo wa mkoa aliyeanza kazi hivi karibuni baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli.
Katika Awamu iliyopita ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete, Anne Kilango alikuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Pia aliwataka viongozi wa halmashauri hizo kuhakikisha wanaongeza kasi ya kukusanya mapato, ikiwa ni sambamba na kuongeza weledi ili mapato hayo yasipotee.
“Maendeleo ya Kahama yanatuhusu wote. Sipendi kumsimamisha mtu kazi kwa tuhuma za ubadhirifu, lakini ikibidi kufanya hivyo nitafanya kulingana na kasi ya uongozi wa Serikali ya Awamu Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli,” alisema.
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na wakurugenzi wa halmashauri 6 za wilaya mkoa wa Shinyanga
=======================================================
NOTA BENE:=======================================================