Nibozali
JF-Expert Member
- Oct 15, 2016
- 572
- 1,055
Kumekucha kila mmoja atafungua na kutoa tathmini kwa wakati wake.
Makinda akosoa sifa za viongozi.
Je, mnakubaliana naye kwa hili? Atumbuliwe asitumbuliwe?
======
Dar es Salaam. Wakati Rais John Magufuli leo akitarajiwa kuongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa kwanza wa Tanganyika baada ya Uhuru, Sir George Kahama, Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda amesema viongozi wa sasa hawana sifa za ulinganinifu na enzi za Mwalimu Julius Nyerere.
Sir George alifariki dunia saa 10:40 jioni ya Jumapili wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), alipokuwa akiendelea na vipimo kwenye kitengo cha dharura.
Mtoto wa marehemu, Anna Kahama alisema mwili wa baba yake utaagwa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere na baadaye utapelekwa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay kwa ajili ya ibada kabla ya kuelekea makaburi ya Kinondoni kwa maziko.
Wengine waliokwenda kuhani msiba jana nyumbani kwa marehemu Mikocheni B ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na kada wa CCM, Sophia Simba aliyefukuzwa uanachama CCM.
Akizungumza na gazeti hili, Makinda alisema tofauti ya viongozi wa zamani na sasa ni kuwa, waliotumikia enzi hizo akiwamo Sir George walikuwa na sifa ya uadilifu na nidhamu ya juu.
Makinda aliyefanya kazi na Sir George, alisema hawakupata wakati mgumu wa kuongoza kwa sababu jamii ilikuwa imejengwa na nidhamu na kwamba, kwa kizazi cha sasa ukionekana unafuata misingi ya sifa hizo, unaonekana umepitwa na wakati.
“Kwa sasa unaweza kuambiwa jambo ambalo hujui limetoka wapi na hakuna anayekanusha,” alisema.
Akimzungumzia Sir George, Sophia alisema ni miongoni mwa viongozi wachache waliotumikia nchi kwa nidhamu, kujituma na kuchangia maendeleo ya Taifa. “Ni mmoja wa viongozi waadilifu, wamefanya kazi kubwa katika Taifa kwa hiyo tunatakiwa kujifunza mengi kutoka kwake,” alisema.
Chanzo: Mwananchi