Uchaguzi 2020 Anna Mghwira atagombea Ubunge?

Oct 7, 2019
51
156
Bado nafikiria kuhusu hekaya ya Mh Rais kuhusu Mwananzila. Kila mtendaji wa Serikali ninayemfikiria angeliisaidia Sana CC
M pale Bungeni kujenga hoja na kunusuru zile mbao za madesk ya binge yasichakae namkumbuka Mwananzila.

Baada ya kuandika kuhusu kiu yangu kwa Prof Kitila Mkumbo na Antony Mtaka Kuingia Bungeni leo tumwangalie Mama Anna Mnghwira. Kwa Sasa tutatumia kanuni ile ile ya SWOT analysis kwa maana ya kuangalia strength, weakness, opportunity,na threats zake ili watu wamfahamu kwa undani.

Strength.
Mama ana Mghwira ana maeneo mengi yenye Ubora lakini Ubora wake zaidi unaweza kuonekana katika maeneo makuu sita.
Moja ni Kati ya wanamama wanaopenda kusoma, Mama Mngwira ni mwanasiasa mwanamke wenye shahada nyingi za Elimu ana shahada ya Thiolojia toka chuo kikuu cha Tumain, ana shahada ya Sheria toka chuo kikuu Cha Daresalam, ana shahada ya Uzamili ya Sheria toka chuo kikuu Cha Essex Uingereza, Mwaka 2018 alitunukiwa Shahada ya Heshima nchini Marekani

Kwa maana hiyo Kama CCM itaamua kumtumia mwanamama huyu Bungeni na katika maeneo Mengine Sina Shaka na uwezo wake wa Kielimu.

Ubora wa Pili wa Mama Mngwira upo katika Uzoefu wa Siasa za Tanzania. Wakati nilipoandika kuhusu Prof Kitila Mkumbo nilisema huenda kinachomsukuma kugombea Ubunge sio mshahara Bali ni kutafuta Self Actualization katika maisha yake. Leo nawaongezea mtu wa Pili ambaye anapenda kufanya Siasa. Mama Mngwira huyu naye Kama akigombea Ubunge si mshahara unamsukuma akagombee Bali ni mojawapo ya watu ambao maisha yao yameathiriwa na kufanya siasa.

Mama Mngwira alianzia Siasa kwenye chama Cha TANU kwenye umoja wa vijana wa TANU (Tanu youth League) Baadaye alikuja kujiunga CHADEMA, na Ni mojawapo ya Mtu aliyeshiriki Kura za maoni Arumeru Mashariki lakini Nassary akapitishwa kugombea Jimbo Hilo.

Akiwa Chadema ameshika nyadhifa mbalimbali Kama Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wilaya na Katibu Baraza la wanawake Mkoa. Baadaye alijiunga na ACT Wazalendo na kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho. Mama Mngwira Ni mwanamama pekee aliyethubutu kushika fomu ya Urais 2015 na kwenye matokeo alishika nafasi ya tatu nyuma ya Rais Magufuli, na Edward Lowasa Kati ya wagombea nane waliochuana.

Kwa Sasa mama Mghwira Ni mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro nafasi aliyoipata 2017 baada ya Rais Magufuli kumteua na katika mazungumzo ya Rais Magufuli baada ya Uteuzi siku ya kuapishwa alisema kwa kinywa chake amechunguza uwezo wake na akajiridhisha kuwa anaweza kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mkoa ambao Ni ngome ya Wapinzani nchini na ndio Mkoa ambao umetoa wenyeviti wa vyama vitatu vikubwa vya Upinzani nchini kwa Sasa. Kwa hiyo kwenye eneo la Uzoefu wa kisiasa hakuna Shaka kuwa huyu Ni nguli haswa na anaijua Siasa ya vyama na utawala vizuri Sana.

Ubora wa tatu wa Mama Mghwira upo katika uthubutu, kama Kuna mtu mthubutu Basi Mama Mghwira huwezi kumuweka kando. Kitendo Cha kuthubutu kuwa mwanamke pekee aliyeshiriki kampeni za 2015 kuusaka Urais Ni Kitendo cha kuigwa na wanawake wote nchini kuacha kutegemea kuwezeshwa Bali waingie katika viunga vya mapambano.

Uthubutu wake umemfanya akawa mtu wa kuhoji, sio mtu wa kukubali kila kitu. Kama Kuna wakuu wa mikoa wadadisi na wenye uwezo mkubwa wa kuhoji mama Mghwira huwezi kumuondoa miongoni mwa tatu Bora.

Uthubutu wake pia umemjengea kujiamini na hata alipopata maambukizi ya Corona alisema wazi wazi bila kuficha na akapambana na ugonjwa Hadi akapona.

Ubora mwingine unaonekana kwenye utulivu wa kutoa maamuzi, imezoeleka kwa wakuu wengi wa mikoa kuwa Ni watu wa media Sana na kutoa matamko, mama Mghwira yeye hana haiba hiyo siku za karibuni kulitokea Jambo la kijamii la mahusiano Kati ya mama wawili na mme wa mtu. Alifanya maamuzi ya Busara Sana na alifikia muafaka wa kuwapatanisha kitu ambacho kingelitokea eneo lingine ingekuwa Ni agenda ya kutumia nguvu za dola.

Utulivu wake huo umemsaidia kutuliza pia Mkoa wa Kilimanjaro ambao Ni Mkoa wa kisiasa na kibiashara kiasilia. Kuongoza Mkoa ambao karibia Halmashauri zote zilikuwa Upinzani na kukabaki na utulivu uliopo na shughuli zikaendelea sio Jambo dogo.

Mwisho kabisa kwenye Ubora mama Mghwira Ni mtu wa kujishusha Sana, kujishusha kwake kunamfanya aweze kujichanganya na kila mtu katika jamii, si ajabu kumkuta mama huyu bila Gari kwenye viunga vya magenge akinunua nyanya na carrot, si ajabu kumkuta na Pochi yake asubuhi kwa miguu akielekea kazini, Si ajabu ukimtembelea nyumbani kumkuta anajipikia Mwenyewe Chakula kwa ajili ya familia yake.

Kujishusha kwake kunamfanya pia kuwa mojawapo ya wakuu wa mikoa ambao Mara Chache anapopata nafasi hupanda kwenye mimbari ya nyumba za Ibada na kulisha watu Chakula Cha kiroho Tukumbuke hapo mwanzo niliwaambia kuwa ana shahada ya Theology.

Weakness
Hakuna mtu mwenye upande mmoja wa shilingi tu, Kama wanadamu wengine Mama Mghwira ana vitu ambavyo Mimi binafsi au watu wengine wanaweza kuviona Kama madhaifu.

Udhaifu wake wa kwanza unaonekana katika kuhama vyama, Mimi binafsi huenda na wengineo linapokuja suala la Imani ya kisiasa naamini kurekebishana ndani ya chama na sio kuondoka. Mama Mghwira mpaka Sasa ameshakuwa mwanachama wa vyama vitatu CCM, ACT, na Chadema. Kuhama huku kunaweza kumsababishia kutokuaminika siku za mbeleni kama atajaribu tena kuondoka CCM.

Udhaifu wake wa Pili unaonekana katika Hali yake ya kuwa mpole mno. Kwa Siasa za Sasa hutakiwi kuwa mpole kwa kiwango Cha mama Mghwira. Kwa wale walio karibu naye wajaribu kumtengeneza kuwa aggressive kidogo Kama anataka kuzimudu Siasa za majukwaani.

Udhaifu wake wa tatu pamoja na utendaji kazi wake mkubwa bado si rahisi Sana kutambua falsafa yake ya maendeleo ipo mrengo gani. Yaani ni vigumu kufahamu mama Mghwira anaamini katika Nini kwenye kuleta maendeleo ya Tanzania. Katika hili anatakiwa ajioambanue zaidi watu wafahamu dira na maono yake katika maendeleo.

Opportunity
Ukiachana na Ubora wake Kuna Mambo ambayo kwake Ni fursa na anaweza kuzitumia.
Fursa kubwa aliyonayo ni Elimu yake, Elimu yake hii si kwamba inamfanya aweze kumudu Majukumu mbalimbali lakini Kama akiitumia vizuri inaweza kumfikisha mbali ndani na njee ya nchi.

Fursa nyingine aliyonayo ni Mwanamke mwenye Nguvu Sana kutokea Kanda ya Kati kwa maana ya mikoa ya Kanda ya Kati. Kama litatokea Jambo la kuwakilisha Kanda hii na anayetakiwa Ni mwanamke Basi Mama Mghwira anaweza Kupata nafasi bila upinzani mkubwa.

Fursa nyingine aliyonayo ukiachana na masuala ya Siasa anaweza kutumika kwenye masuala ya Kidiplomasia. Japokuwa hajaisomea lakini ana Diplomasia ya kuzaliwa, mama huyu anaweza kutusemea vizuri Sana njee ya mipaka yetu na tukavuna Elimu yake ambayo hatujaifaidi Sana.

Threats
Kuna vitu vichache ambavyo Ni tishio kwake vinavyomzunguka.

Moja haikulikani Kama anataka kugombea wapi, Kilimanjaro au Nyumbani Singida. Pamoja na kwamba kote anaweza kushinda lakini anatakiwa Sasa achore mstari watu wafahamu na Kama Ni ground work ifanyike. Kwa wagombea wengi mpaka Sasa walishatambua na wananchi walishajua wenye nia katika majimbo yao.

Tishio la Pili ni ile hadithi ya Mwananzila. Je Rais atamruhusu kwenda kugombea? Kama atagombea bila ruhusa Nini kitatokea baada ya Kushindwa. Hapa panahitaji hesabu kubwa kabla ya kwenda.

All ni all kila la Kheri Mama Yetu Anna Elisha Mghwira wewe ni mtu wa tatu ninayetamani nikuone kwenye viunga vya Bunge letu.
ANNA.jpg
 
Mkuu naona umemaliza, ingawa hujaweka space katika andiko lako ila limeeleweka
 
Usisahau yuko kazini paze zake zote !!! Ndio wale wale... Kikazi zaidi
 
Uchambuzi mzuri. Kwenye upole na diplomasia yuko vizuri. Kuna DC mmoja kwenye mkoa anaouongoza ni mtata hasa. Upole wake unaombatana na hekima na kutumia diplomasia kumesaidia aweze kummudu vilivyo huyo DC.
 
Aliwahi kuhojiwa na kipindi cha star tv nkashangaa imekuwaje mkula kampa u RC mtu ambaye hajui kujieleza .

ukiona mwanasiasa anatoka ccm, anaenda chadema au kuhama chama chochete cha siasa huyo sio mwanasiasa

mwenzetu wako karne 21 sisi bado tupo karne pendwa 18 tukipeana vyeo, na madaraka
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom