Anguko kuu la CHADEMA

Mbona kama unatufokea tukubali unachosema haya ni kweli kitasambaratika na akifuati sheria ya natural justice na ni cha ajabu sana ingawa ulikipenda sasa si ufurahi nini kutufokea
 
Pengine wewe ndiyo utaanguka, Chadema Ni chama pekee katika ukanda huu wa Afrika Mashariki inayopambana na vitisho vya Kila aina lakini bado inapumzi ogopa. Polisi, nadhani unawaelewa vizuri, wameifanya watawala wasilale usingizi.

Wewe Kama unataka kupima uwezo wa Chadema Mbowe aongee tu utawasikia viongozi wale wasiotulizana wakikimbizana kumjibu. Sasa hivi Gwajima naye ameachana kumnanga shetani na kugeukia kulaani Chadema. Nenda polisi useme Chadema Wana mkutano utaona magari ya washa na hata Yale mabovu yakitumuka mbio halafu eti useme anguko!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utaanza kuanguka wewe kabla ya CHADEMA si umeona Wassira alisema CHADEMA itakufa ameanza "KUFA' yeye kabla ya CHADEMA,
 
Chadema ni genge la wakora likiongozwa na Mbowe ,ni wakuogopwa kama ugonjwa wa ukoma ,hili genge lidisapie tu hata kwa kuvunja sheria za nchi ,likiachwa madhara yake ni makubwa sana kwa taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
Inabidi msajili wa vyama vingi aliangalie hili suala kwa mapana na kwa maslahi ya Jamii.
 
Hivi ukimkataza mtoto wako asifanye jambo fulani halafu yeye akiwa na alili zake timamu kabisa akafanya, wewe kama mzazi utatoa muda wako umsikilize kwanini amefanya?

Hao wabunge baada ya kukatazwa ni kwanini wasinge protest pale pale kuonesha hawajaridhika na maamuzi ya kuwazuia wasiende bungeni? Tafsiri inayokuja hapo ni kwamba wamekaidi agizo halali la chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikundi, kusanyiko ama jumuia yoyote lazima iwe na miiko, misingi na itikadi zake...

Na huwezi kwenda kinyume au kuivuruga kwa makusudi ama kwa manufaa yako halafu uachwe hivi hivi...
Ukiona unaachwa bila kuwajibishwa ujue hiyo jumuia ni sawa na mfu!

Hapa mtaongea sana lakini ifahamike wazi kuwa unakuwa huru unapokuwa mtu peke yako...!!
Ukishaamua kujiunga na watu fulani lazima vigezo na masharti vizingatiwe...!!

Unapolalamikia vitu ambavyo viko wazi ndani ya jumuia yenu tena kwa wasio wanajumuia inaonesha wazi kuwa wewe kama mwanajumuia ndo una matatizo makubwa sana ya akili na maadili...!!

Anyway politicians karibia wote ni con-artists... Usiwaamini na wala usiweke matarajio makubwa sana juu yao...
 
Jipu la jirani linapokukera,lini ccm watajenga nchi bila kukumbuka timbwili za upinzani?

Jenga uchumi imara,miundombinu ya usafiri, afya, elimu, maji na kuwe na usalama wa watu kutoa maoni....
Uone huo upinzani utaanzaje kuwatisha.

Kwa hali hii hata mwana CCM akivaa nguo yenye rangi zinazoshabihiana na za vyama vya upande huo, mashavu yatawajaa bila hata sababu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Naona kuelekea uchaguzi mkuu mmejazwa humu ndani kujibu mashambulizi, lakini hali yenu itakuwa ngumu sana.
 
Naona kuelekea uchaguzi mkuu mmejazwa humu ndani kujibu mashambulizi, lakini hali yenu itakuwa ngumu sana.
Sasa si unaona mawazo yenu yalivyo...mtu akiwa against nanyi katumwa...kwamba huwa mnatenda kwa usahihi siku zote...Mtazamo mbovu kabisa
 
Nenda kawaulize watabiri wenzako wa kifo cha Chadema, tangu walipoanza kutabiri miaka mingi iliyopita je ,Chadema imekufa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
How much are you paid for such a nonsense ?
 
Hizi ramli ziliasisiwa na mzee Wasira, nyie wengine fuata upepo tu.
Toka hizi porojo zisemwe ni muda sasa lakini CDM ipo tu. Itoshe tu kusema kuwa cdm ni chama kubwa na haliwezi kuisha. Wanatoka lakini lipo tu,hata kama hukipendi lazima ukikubali tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…