Anguko kuu la CCM laanzia Butiama jimbo jipya

BABA ERIZA

Member
Jan 7, 2015
79
12
Wanajukwaa,

Ikiwa viongozi wakuu wa ukawa wako kwenye hatua za mwisho kumleta Rais anaesubiliwa na umma mzima wa Tanzania, wananchi jimbo la butiama na Mara kwa ujumla wameendelea kusema wazi wazi kuwa mabadiliko hayo ya kulikomboa taifa sasa yataanzia butiama, ambapo wengi wao wameshangazwa na kitendo cha ccm kuendelea kuleta wagombea walioshirikili kugawa mali za umma mithili ya karanga, wakienda mbali na kuhoji tangu lini mtu kama Magufuli alihusika kwenye uuzwaji wa nyumba za serikali ambazo zilijengwa kwa jasho la watanzania maskini leo aletwe na kupigiwa kengele eti ana usafi wa kuwa rais wa Tanzania, wamesema haiwezekani.

Kwa sauti yao ya kipekekee wamemwambia mbunge Nimrod asidhubutu hata kuchukua fomu maana asubuhi tu watamwangusha vibaya, wanahoji Mkono ameshiriki kupora Fedha kiasi kikubwa cha fedha zilizotolewa na Umoja wa Ulaya kujenga Chuo kikuu cha Nyerere na akazigeuzia Fedha hizo kama Mradi binafsi ambao alijenga Shule mbili na kuziuzia Serikali kwa Faida kubwa kwa maslai binafsi hivyo kusababisha uwezekano wa Chuo hicho kuwepo kuwa ndoto, maana ikilazimishwa majengo ya Shule hizo ndiyo yatabadilishwa tena kuwa majengo ya Chuo, hii ni fedheha, hivyo hadi sasa jimbo la Butiama CCM hawana mtu yeyote atakaethubutu kuchukua fomu labda achukue kiushahidi kusubiri anguko lake na CCM kwa ujumla.

Kwa sasa macho yote yako kwa Makamanda 6 waliojitokeza kwa tiketi ya CHADEMA na nitawaweka hapa na wasifu wao ili wanabutiama na watanzania kwa ujumla tuwafahamu na endapo mmoja wao akipewa ridhaa tumunge Mkono kwa maslai ya taifa.

1. Daniel Obiya - Shahada ya kwanza ya Ualimu

2. Yusuph Kazi - Kidato cha nne, Mfanyabiashara

3. Marwa Marato - Shahada ya Uzamili, afya ya Umma

4. Gabriel Gebo - Kidato cha nne, Mfanyabiashara

5. Issa Yusuph - Shahada ya kwanza ya Ualimu

6. D. Okielo - Shahada ya Ualimu

Ndugu, wanabutiama na watanzania tuwapime na kuwaunga mkono ili mmojawao awe mwakilishi sahihi na wa kusimamia maendeleo ya jimbo la butiama kiufasaha, Tuwajadili kwa staha na utu ili tuwafahamu zao kabla ya muda wa kumpata mmoja wao.
 
Unawasemea watu wa Butiama..................
Tukutane kwenye sanduku la kura
 
Mkono na CCM kwa miaka kumi walishindwa kuwasemea ndo maana UKAWA wako tayari kuwakilisha na kutatua changamoto kwa vitendo
 
Mkuu Nimrodi Mkono ni wa Musoma Vijijini hilo jimbo jipya la Butiama watagombea wengine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom