Angetile osia ameshindwa kuongoza tff | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angetile osia ameshindwa kuongoza tff

Discussion in 'Sports' started by kazikubwa, Sep 11, 2012.

 1. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama kuna mtu ameandika historia mbaya ya uongozi wa soka hapa nchini ni huyu bwana. Katika kipindi chake akiwa kama katibu ameshindwa kuwa thabiti na kusababisha migongano ya hapa na pale kati ya Klabu na TFF au kati ya Klabu na Klabu.

  Matatizo aliyosababisha kwa uchache ni kama yafuatayo:
  1. Kukosekana kwa waamuzi thabiti wa soka na kupanga waamuzi hasa wa mechi za Yanga kwa upendeleo
  2. Kuwepo kwa usimamizi mbaya wa soka na fedha za TFF
  3. Kuwa na maandalizi duni kwa timu zetu za Taifa

  Na wenzangu ongezeeni hapo chini. Cha msingi kwake ni kujiuzulu ili kuleta imani kwa wapenzi wa soka na kujijengea heshima kabla ya kulazimishwa kufanya hivyo.
   
 2. Mdakuzi

  Mdakuzi JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,748
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280

  Kinachomlinda huyu jamaa ni kufanyakazi na waandishi wa habari kwa kipindi kirefu akiwa ni Mhariri, na ndio maana wanashindwa kumwandika mwenzao. Na hii ndio sababu hasa ya akina Tenga kumweka hapo ili kuzima madudu yao yasitoke magazetini, ila huyu jamaa ni kimeo hasa.
  Hebu ona hata tatizo la ucheleweshaji wa ratiba ya ligi kuu, wakati ndio kazi kuu ya TFF ukiondoa maandalizi ya timu ya Taifa, inayoendelea kuporomoka kwenye viwango kila kukicha.
  Jambo la muhimu alilofanya tangu aingie madarakani ni yeye kwenda kutibiwa India kutokana na matatizo ya kichwa, lakini mambo mengine yote amekuwa akichemsha tu, na hakuna wa kumkosoa kwani kila mwandishi ni rafiki yake au vijana wake aliokuwa akiwatuma kazi alipokuwa mhariri.
   
 3. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,366
  Likes Received: 488
  Trophy Points: 180
  Sijafanya uchunguzi sana lakini naweza kukubaliana na wewe kwa kuwa moja kati ya sifa kuu za uongozi mbovu ni migogoro isiyoisha
   
 4. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  poa nami nakubaliana na wewe jamaa hili ni mzigo mkubwa sana tff ila mkataba wake unaisha january 2013 sizani kama ataongezewa mkataba mwingine na rais ajae.
   
 5. p

  pilau JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Niliwahi kuuliza huyu jamaa amepataje Ukatibu mkuu wa TFF? Nadhani ni moja ya MAAJABU yaliyowahi kulikumba Soka la bongo ambalo hatutalisahau maisha ni Angetile kuwa katibu mkuu wa TFF ......... Mimi naungana mkono na wewe kabisa kama nchi hii ina watu walioshindwa na hawafai kuongoza sekta zinazohusiana na jamii jamaa huyu anaongoza, jamaa anapwaya sana ni mwepesi, na anaonyesha kuwa na maslahi binafsi na klabu ya Yanga, sikatai mapenzi ya mtu, lakini kwa Angetile ni bomu kwa hali yoyote hawezi kugombea tena mkataba wake ukiisha na akarudi madarakani,
   
 6. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Sijafanya uchunguzi ila wewe ni shabiki wa SIMBA.
   
 7. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi natofautiana na wengi hapa.Labda tujiulize maswali kwamba Angetile ameshindwa kuongoza TFF kama Entity au ameshindwa kuongoza soka la Tanzania kama sector.Kwa sababu unapoongela failures za TFF huwezi kuacha kuongelea failures kwa soka la Tanzania.Na kwa maoni yangu mimi kushuka(failures) za soka la TZ/TFF ni mfumo zaidi kuliko mtu mmoja na kwa watu ambao tupo kwenye soka la Tanzania tunaweza sema TFF kuna transparency zaidi kuliko kipindi chochote nilichokiona,lakini hii inawezekana kutoka na kipindi tulichopo.
  TFF ipo kwa kushirikiana na serikali kuendeleza policy(kama zipo) za kuendeleza na kunyanyua kiwango cha soka letu,vitu kama michezo ya UMITASHUTA,UMISETA ndio ilikuwa chimbuko la wanamichezo wetu sio kwa soka tu hata michezo mingine.
  Kwa hiyo nafikiri tusiangalie tu failures za Angetile kama yeye bali TFF kama chombo kwa upande mmoja na serikali kwa uapnde mwingine.Na tuache ugonjwa tulio nao waTanzania wa Usimba na UYanga
   
 8. M

  Masikrodinga JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 229
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kaka 2naanzia kwa TFF then ndo SOKA kwa ujumla, kifupi Osiah kabla hajaingia TFF alikuwa mbele kuipgia kelele taasisi hii lakn alipopewa mwana alee AIBU TUPU. Kwanza hajiheshim akiwa kama kiongozi wa TFF, hatukatai kuwa inawezekana karibia kila Mtanzania ana itikadi yake ya Usimba na Uyanga lakn unapopewa dhamana ya kuongoza taasisi kama TFF jaribu kuwa na busara kidogo. Angetile Yanga ikishinda akifika Bar anamwaga ofa huku anatamka maneno ya kishabiki kwa Yanga. Osiah haingii hata robo ya uwezo wa katibu aliyemtangulia, Mwakalebela.
   
Loading...