Nina rafiki yangu ambaye tumeshibana saana kwa kauli nyingine sio rafiki tena ni ndugu kabisa.
Huyo rafiki yangu baba yake ni mgonjwa saana anaumwa sana. Tulikwenda naye hospitali wakasema anahitaji kufanyiwa upasuaji tumboni mwake na hili afanyewe hivo kuna pesa fulani ambazo wanaomba hili apate kutibiwa.
Sasa kuna pesa ambazo nilipewa na familia yangu baada ya dada zangu kuolewa wazazi wakaona zile pesa tufanye nazo biashara wakanipa mimi kama mtoto wao wa kiume. Na kwenye plan yangu ya biashara nilikuwa nipo na huyu ndugu yangu (rafiki) tulikuwa tuna panga wote.
Sasa baada ya baba yake kuumwa hizo pesa anaomba eti ni msaidie hili amtibishe baba yake najaribu kumwambia nitampa nusu kwa bahati mbaya nusu nyingine hana kwa hiyo anaomba pesa zangu eti Mungu atanilipa utu wa mtu ni muhimu kuliko pesa. Na kweli mzee wake ni mgonjwa saana na asipo tibiwa mapema ni Mungu tu
Mimi na shindwa na la kufanya kabisa
Yaani sijui nikimpa wazazi nitawapa taarifa gani au nitapata wapi tena pesa zingine. Nahisi na changanikiwa kabisa
Naona sina bahati kabisa.
Sijui naombeni ushauri
Kwanza pesa si yako. Naye anafahamu hilo. Mweleze muende kwa wazazi na ndugu waliokupa huo mtaji watoe uamuzi. Hii itakuepusha na lawama kwake na waliokukabidhi huo mtaji. PESA SI ZAKO.Nina rafiki yangu ambaye tumeshibana saana kwa kauli nyingine sio rafiki tena ni ndugu kabisa.
Huyo rafiki yangu baba yake ni mgonjwa saana anaumwa sana. Tulikwenda naye hospitali wakasema anahitaji kufanyiwa upasuaji tumboni mwake na hili afanyewe hivo kuna pesa fulani ambazo wanaomba hili apate kutibiwa.
Sasa kuna pesa ambazo nilipewa na familia yangu baada ya dada zangu kuolewa wazazi wakaona zile pesa tufanye nazo biashara wakanipa mimi kama mtoto wao wa kiume. Na kwenye plan yangu ya biashara nilikuwa nipo na huyu ndugu yangu (rafiki) tulikuwa tuna panga wote.
Sasa baada ya baba yake kuumwa hizo pesa anaomba eti ni msaidie hili amtibishe baba yake najaribu kumwambia nitampa nusu kwa bahati mbaya nusu nyingine hana kwa hiyo anaomba pesa zangu eti Mungu atanilipa utu wa mtu ni muhimu kuliko pesa. Na kweli mzee wake ni mgonjwa saana na asipo tibiwa mapema ni Mungu tu
Mimi na shindwa na la kufanya kabisa
Yaani sijui nikimpa wazazi nitawapa taarifa gani au nitapata wapi tena pesa zingine. Nahisi na changanikiwa kabisa
Naona sina bahati kabisa.
Sijui naombeni ushauri
Dah mzee umezungumza kitu cha maana ila watu hawatakuelewa ,maisha haya kila kitu fanya kwa kiasi ,usifanye jambo ukapitiliza mpaka ukajinyima kila kitu kwa ajili ya mtu mwingine ambaye hatokuja jinyima kwa ajili yako ,utaumia sana mbeleni huko ,binaadamu sio wa kuwaaamini kabisaaaaUkimpa hela rafiki yako urafiki umeisha, na usipo mpa hela urafiki umeisha. Uchaguzi ni wako ufanyie biashara au umpe rafiki yako awe adui yako. Rafiki yako ana familia yake wakae kitako watatuwe shida zao sio wewe ubebe shida zao. Kwani wao wamewahi kukusaidia nini??
Kama hyo pesa ni kubwa huwezi kuipata wewe kama wewe kwa haraka kweny hustling zako usimpe..Tambua ana ndugu kibao mgaiye kidogo ,urafiki unakufa pia ..
Mfano kama pesa ni million 10 mpe hata million 1 au mbili usitoe pesa ndefu...huyo mzee ana mtoto mmoja pekee? baadhi ya marafiki haswa wabinafsi ni wajanja sana .
Watu wabinafsi haswa marafiki utawagundua kupeleka shida zake mbele kweny upande wake haswa kweny ishu za pamoja ..Kama hapo alitakiwa kujua kwamba ishu ya mzee wake ni yake private sio kuileta kwa rafiki yakeMarafiki huwa wabinafs mno tena wakikuona una roho nzuri Ndio wanatake advantage