Angalizo kuhusu biashara ya mtandao (Network Marketing)

Angalizo kuhusu biashara ya mtandao (Network Marketing)

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,914
Reaction score
3,437
Habari rafiki,
Nimekuwa nawashauri watu ambao wanataka kuingia kwenye biashara na hawajui pa kuanzia basi waingie kwenye biashara ya mtandao (network marketing).

Huu ni mfumo bora kabisa wa kibiashara ambapo mtu anajifunza mengi kuhusu biashara ikiwa ni pamoja na kunadi biashara yako, kujenga timu na kujiamini.

Lakini pia kuweni makini na hizi kampuni zinazochipukia za biashara hiinya mtandao, nyingi siyo halisi.

Nikupe vitu vitatu muhimu vya kuangalia kabla hujaamia kuingia kwenye biashara ya mtandao unayoambiwa inalipa vizuri;

1. Biashara iwe na bidhaa au huduma ambayo watu wanaihitaji na wapo tayari kulipia.

2. Uwe unalipwa kutokana na faida inayopatikana baada ya watu kununua bidhaa, na siyo ulipwe kwa kuwaingiza watu pekee.

3. Anayekuambia uingie kwenye biashara fulani ambayo yupo yeye akisema inalipa, mwambie kwanza akuoneshe ushahidi wa yeye kulipwa cash, kama hajawahi kulipwa cash ila anaambiwa tu ana hela zake zipo kwenye mfumo, kimbia haraka sana,huo ni utapeli.

Neno la mwisho kwakp rafiki, hakuna biashara rahisi, hakuna njia ya haraka ya kupata fedha ambayo haikutoi jasho la mwili au akili. Usipoteze muda wako kwa mambo ya utapeli.
Weka juhudi kwenye biashara sahihi na utafanikiwa.

#MUHIMU; Naandika kitabu kuhusu BISHARA YA MTANDAO, mambo yote muhimu mtu anayopaswa kuyajua. Kama una swali kuhusu biashara hii au una kampuni ambayo ungependa kuijua kwa undani niandikie swali lako kwenye email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Rafiki na kocha wako,
Makirita Amani,
www.makirita.info
 
Ahsante Mkuu lakini je, unafahamu nini kuhusu hawa watu wa Forever living??
Forever ni biashara halali ya mtandao.
Ina bidhaa zinazohitajika na watu.
Unalipwa kulingana na faida ambayo kampuni imepata kwa watu kununua bidhaa.
Kuna ushahidi wa watu kulipwa hela zao cash.
 
Alliance global in motion uko vizuri
Zaidi . na evidence za bank statements za watu wanaotengeneza million 200 kwa miezi miwili zipo, wa wana miaka miwili tu wamejoin kwenye kampuni
 
Back
Top Bottom