Hivyo,waliohitimu udsm wako kwenye ajira?... kwa kuwa ni chuo bora zaidi Tanzania.
Au waliohitimu Tanzania international university hawana ajira? Kwa kuwa ni chuo kisicho bora Tanzania.
Mwisho wa siku,maji ufata mkondo... Mwenzio anamaliza Eckernforde Tanga university unamkuta ni afisa wa jeshi,wewe na degree yako ya udsm unalia ajira.
Siku hizi pesa haiongei pesa ina apa... Mwenzako anaambiwa kasome tu chochote mwanangu ajira ni kuhonga tu,wewe unatafuta kozi za kipaumbele na unarudi kusugua kitaa.
Ajira ni kitendawili... Hakiangalii wewe ni kutoka udsm au teku... Ukiwa na pesa,bahati na channel basi utapata.