Angalia Data za World Bank; Nani Zaidi - Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli Kwa Uchumi Tanzania

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,639
22,490
upload_2017-1-27_14-59-25.png

Labda hiyo graph haoinekani vizuri, lakini inachoonyesha ni kwamba kulingana na data za Benki ya dunia, tukitumia GDP per capital growth rate, katika kipindi cha Mwinyi, Mkapa na JK, Mkapa ndio aling'ara kwenye kuinua ukuzi wa uchumi, tunapolinganisha alipoingia na alipotoka, na kwa ujumla.

Japo kwa Mwinyi tunachoona ni miaka yake mitano ya mwisho - inaonyesha aliuacha uchumi katika hali mbaya kuliko kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano. Mwinyi peke yake aliingiza Tanzania kwenye negative GDP per capital growth rate, hadi wastani wa -3%.

Mkapa alipochukua nchi aliuboresha uchumi zaidi sana ya Mwinyi alipouacha. Kuelekea mwishoni mwa kipindi cha Mkapa kasi ya ukuzi ilipungua, labda ni kipindi kila mtu alianza kuchukua chake! Kwa ujumla ukuzi wa uchumi wakati wa Mkapa ulikuwa na msimamo mzuri unaoeleweka, sio panda shuka ya Mwinyi na Kikwete.

Kikwete alipochukua toka kwa Mkapa ghafla uchumi alianza kuporoka chini zaidi ya pale alipouacha Mkapa. Jambo lililo wazi ni kwamba wakati wa Kikwete ukuzi wa uchumi ulikuwa hauna msimamo kamili, kila mwaka kupanda na kushuka kuonyesha Kikwete hakuwa na mwelekeo unaoeleweka katika mambo ya uchumi ukilinganisha na Mkapa. Kwa wastani Kikwete aliushusha uchumi kuliko alipouacha Mkapa.

Katika kipindi cha mwaka mmoja cha JPM, japo watu wanalalamika kwamba shilingi imeota miguu, lakini yeye amefikia rekodi ya GDP per capita growth rate ambayo haijawahi kufikiwa na maraisi wote waliomtangulia. Magufuli alipochukua tu nchi toka kwa Kiwete tulianza kupanda. Sasa hii inamaanisha nini kuelekea mbele tunasubiri kuona, na mwishoni mwa 2017 tutapata picha kamili.

Ila picha ya ujumla ni kwamba tangu 1990 hadi 2016 tumeenda vizuri sana. Katika kipindi cha Mwinyi na Kikwete kwa wastani hatukwenda mbele wala kurudi nyuma. Hadi sasa ni Mkapa peke yake aliyetuinua tangu mwaka 1990. Na Magufuli anaonekana ana mwelekeo wa kutuinua toka pale alipotuacha Mkapa.

NB. Data za 2016 kipindi cha JPM hapo juu ni halisi, isipokuwa zimefanywa wastani wa quarter tatu (January - September), Q1, Q2, Q3, badala ya nne za miaka mingine.

Source: GDP per capita growth (annual %) | Data
 
Tatizo la world Bank wanaangalia upande mmoja tu wa uchumi kukua kwenye makaratasi................

Huwezi kuongelea uchumi bila kuangalia per capital income.........


Mwinyi ndiye alifanikiwa kujenga uchumi hasa uchumi Wa watu.........

Unapojenga uchumi Wa watu na ukawekeza kwenye elimu Afya na infrastructure lazima Uchumi Wa nchi utakuwa mkubwa..............
 
Angalia mambo yalivyo SA; Mbeki ndiye aliyeipaisha South Afrika kuliko maraisi wote, na Zuma ndio kaharibu kuliko wote!
upload_2017-1-27_12-17-55.png
 
vitu gani hasa huangaliwa kabla ya kusema uchumi umekua au la? inawezekana more than 80% ya wananchi wako hoi kiuchumi na still ikawa declared kwamba uchumi wa nchi umekua?
 
View attachment 464251


Labda hiyo grapgh haoinekani vizuri, lakini inachoonyesha ni kwamba kulingana na data za Benki ya dunia, tukitumia GDP per capital growth rate, katika kipindi cha Mwinyi, Mkapa na JK, Mkapa ndio aling'ara kwenye kuinua ukuzi wa uchumi, tunapolinganisha alipoingia na alipotoka, na kwa ujumla.

Japo kwa Mwinyi tunachoona ni miaka yake mitano ya mwisho - inaonyesha aliuacha uchumi katika hali mbaya kuliko kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano.

Mkapa alipochukua nchi aliuboresha uchumi zaidi sana ya Mwinyi alipouacha, japokuwa mwishoni mwa utawala wake kuelekea uchaguzi mkuu uchumi ulianza kuporomoka tena - labda watu wakiwahi kuchukua chao! Ukuzi wa uchumi wakati wa Mkapa ulikuwa na msimamo mzuri unaoeleweka, sio panda shuka ya Mwinyi na Kikwete.

Kikwete alipochukua toka kwa Mkapa mwanzoni alirekebisha sana mporomoko uliotokea mwishoni mwa Mkapa, lakini ghafla alianza kuuporomosha chini zaidi ya pale alipouacha Mkapa. Jambo lililo wazi ni kwamba wakati wa Kikwete ukuzi wa uchumi ulikuwa hauna msimamo kamili, kila mwaka kupanda na kushuka kuonyesha Kikwete hakuwa na mwelekeo unaoeleweka katika mambo ya uchumi ukilinganisha na Mkapa. Kwa wastani Kikwete aliushusha uchumi kuliko alipouacha Mkapa.

Katika kipindi cha mwaka mmoja cha JPM, japo watu wanalalamika kwamba shilingi imeota miguu, lakini yeye amefikia rekodi ya GDP per capita growth rate ambayo haijawahi kufikiwa na maraisi wote waliomtangulia. Magufuli alipochukua tu nchi toka kwa Kiwete tulianza kupanda. Sasa hii inamaanisha nini kuelekea mbele tunasubiri kuona, na mwishoni mwa 2017 tutapata picha kamili.

Ila picha ya ujumla ni kwamba tangu 1990 hadi 2016 tumeenda vizuri sana. Ila katika kipindi cha Mwinyi na Kikwete kwa wastani hatukwenda mbele wala kurudi nyuma. Hadi sasa ni Mkapa peke yake aliyetuinua tangu mwaka 1990. Na Magufuli anaonekana ana mwelekeo wa kutuinua toka pale alipotuacha Mkapa.
Upumbavu mtupu
 
Kutokana na takwimu zako, mambo inaonekana yalikua mazuri kipindi cha mkapa na ndicho kipindi ambacho serikali iliweka juhudi Kubwa katika kukusanya kodi!

Hivyo hivyo kipindi hiki cha Magufuli hakina tofauti sana na cha Mkapa ila kitakuwa kizuri zaidi kwani ukiachana na makusanyo ya kodi, Rais amewekeza katika Sera ya viwanda ambayo kama ikisimamiwa vyema itaongeza ajira kwa wananchi na mapato zaidi kwa serikali, swala ambalo litapelekea kuboreshwa kwa Huduma za kijamii kama afya, miundombinu na elimu!

Ingawa Sera ya viwanda ni muhimu, ila sio vibaya kwa serikali kuboresha sekta ya kilimo na ufugaji ambayo hiyo itawagusa wananchi wengi sana ambao wanategemea kuendesha maisha yao kwa kutegemea shughuli hizo!
 
Back
Top Bottom